Michango kwa ajili ya kufanikisha shughuli za msiba wa Marehemu Mama Harriette Peace Kagaruki aliyefariki dunia huko Philadelphia tarehe 28 April 2014 imekamilika. Mpaka sasa kiasi cha dolla 20,000 kimepatikana kama ifuatavyo:

·      Watanzania Marekani wametoa dolla 5,300
·      Familia, ndugu na Jamaa wa Tanzania wametoa dolla 11,000
·      Watoto wa Marehemu Erick na Mary Kagaruki wametoa kiasi kilichobakia cha dolla 3,700.
 
Watoto wa Marehemu Erick Kagaruki na Mary Kagaruki na familia nzima ya Marehemu mama Harriette Peace Kagaruki wanapenda kuwashukuru wote mliotoa michango, rambirambi na mliofanikisha kwa namna moja au nyingine shughuli hizi za msiba ziweze kufanikiwa.
 
Shukrani nyingine ziende kwa Watanzania wote na rafiki wa Watanzania waliochangia shughuli za msiba huu hapa Marekani na Tanzania.
 
Mwili wa Marehemu umeshaletwa New Jersey kutoka Philadelphia tayari kupelekwa Tanzania siku ya Jumanne usiku saa tatu kupitia airport ya Newark na British Airways via Entebbe.
 
Mwili utawasili Entebbe Jumatano kabla ya safari ya kuelekea Bukoba kuanza kwa ajili ya shughuli mazishi kuanza.
 
Familia inapenda tena kuwashukuru wote kwa kufanikisha michango na shughuli za sasa za msiba huu. Tunawaomba Watanzania wote tuendelee kushirikiana katika nyakati za shida na raha kama tulivyoshirikiana wakati huu wa msiba.
 
Kwa taarifa zaidi wasiliana na:
Erick Kagaruki – 937-361-4189
Mary Kagaruki – 267-963-8190
Abbas Byabusha – 914-584-7502
   
Kwa niaba ya Familia ya Wafiwa na 
Uongozi wa Jumuiya ya Watanzania,
 
Deogratius Mhella, 
Katibu New York Tanzanian Community.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 11, 2014

    Watanzania owte mliojitoa kufanikisha zoezi ili Mungu wetu awabariki sana. Ninaomba tu niwakumbushe wote kwamba kushirikiana ni jambo la muhimu sana. Kila mtu mahali ulipo ndipo nyumbani kwa hivyo ni vizuri kutafuta ndugu huko uliko. Ajabu msaada mkubwa umetoka Tanzania. Jifunzeni kitu ndugu zangu, mpendane, mtafutane, mshirikiane. Mkipata shida au furaha mbebane. Acheni kuwa busy. Maana wasawahili tunasema kutesa kwa zamu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...