Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nayalandu, akisainiana mkataba wa makabidhiano wa magari matatu aina ya Land Cruiser, yenye thamani ya Sh. milioni 350, na Mwenyekiti wa Taasisi ya Uhifadhi Wanyamapori Tanzania, Eric Pasanisi (wa pili kushoto) wakati wa hafla ya makabidhiano hayo iliyofanyika leo kwenye Hoteli ya Hyatt Kilimanjaro wakati wa Kongamano la Kampeni ya kudhibiti Ujangili na kukomesha mauaji dhidi ya Tembo. Kongamano hilo lililofunguliwa na Makamu wa Rais Dkt Bilal, jana limemalizika leo Mei 10, 2014. Kushoto ni Naibu Spika wa Bunge la Jamhri, Job Ndugai (kulia) ni Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mahmoud Mgimwa
 Wakibadilishana nyaraka za mkataba huo baada ya kutiliana saini. Kushoto ni Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri, Job Ndugai
 Baadhi ya washiriki wa Kongamano la Kampeni ya kudhibiti Ujangili na kukomesha mauaji dhidi ya Tembo, wakiwa katika Kongamano hilo, lililomalizika leo kwenye Hoteli ya Hyatt Kilimanjaro, jijini Dar Es salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...