Wanafunzi wa elimu ya awali, wakifundishwa na mwalimu Juliana Joseph huku wakiwa wamekaa sakafuni na juu ya paa kukiwa wazi katika moja ya vyumba vya madarasa ya Shule ya Msingi, Unyaghumpi vilivyozuiliwa kujengwa na Mbunge Tundu Lissu kwa kuwakataza wananchi kuchangia fedha na kuwaambia kuwa fedha zote zitatoka serikalini,imeelezwa na Wananchi wa jimbo hilo kuwa kufuatia na hali hiyo miradi mingi imekwama kwa miaka minne sasa,jambo ambalo limewarudisha nyuma kimaendeleo.
 Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akisaidia kuvuna mtama na uwele kwenye shamba bibi mjane asiye na mtoto, Mayasa Mkhandi katika Kata ya Unyaghumpi, Jimbo la Singida Mashariki, mkoani Singida,wakati wa ziara yake ya kuimarisha uhai wa chama, kukagua, kuhimiza na kusukuma ujenzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya CCM, kukagua maandalizi ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na kusikiliza kero za Wananchi na kuzitafutia ufumbuzi. 

Katika Jimbo hilo linaloongozwa na Mbunge Tundu Lissu wa Chadema, Kinana alishuhudia miradi mbalimbali ya maendeleo ambayo ujenzi wake umekwamishwa na mbunge huyo kwa kuwzuia wananchi kuchangia fedha za miradi hiyo akidai kuwa fedha zote zitatoka serikalini.

Baadhi ya miradi iliyosimama aliyoikagua Kinana, ni Zahanati ya Kimbwi ukiwemo ujenzi wa nyumba za waganga ambayo imeishia kwa kupigwa msingi wa zege. Vyumba vya madarasa vya shule ya msingi Unyaghumpi ambapo walikutwa watoto wa shule ya awali wakifundishwa huku wakiwa wamekaa sakafuni na juu kukiwa wazi bila kuzekwa. Miradi mingine iliyokwama ni ujenzi wa barabara, mawasiliano ya simu, maji na umeme.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia katika mkutano wa hadhara ulofanyika  katika Kijiji cha Makiungu, wilayani Ikingu, Jimbo la Singida Mashariki la Mbunge Tundu Lissu wa Chadema. Kinana alimponda Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki kwa kitendo chake cha kuwakataza wananchi kuchangia fedha za miradi maendeleo na kusababisha jimbo hilo kudorora kimaendeleo tofauti ma majimbo mengine nchini. Alisema badala ya kuwasaidia wananchi badala yake anaendekeza masuala ya UKAWA na kutukana matusi bungeni.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia katika mkutano wa hadhara ulofanyika  katika Kijiji cha Makiungu, wilayani Ikingu, Jimbo la Singida Mashariki la Mbunge Tundu Lissu wa Chadema. Kinana alimponda Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki kwa kitendo chake cha kuwakataza wananchi kuchangia fedha za miradi maendeleo na kusababisha jimbo hilo kudorora kimaendeleo tofauti ma majimbo mengine nchini. Alisema badala ya kuwasaidia wananchi badala yake anaendekeza masuala UKAWA na kutukana matuzi bungeni.
Aliyekuwa kiongozi wa Chadema, Ismail Gwau, akitupilia mbali bendera ya CHADEMA mara baada ya kutangaza kujiunga na chama cha CCM,katika Mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye stendi ya mabasi mjini Ikungi.
Sehemu ya Wakazi wa Ikungi wakishangilia jambo kwenye mkutano wa hadhara.
Mmoja wa Viongozi wa CCM,Wilaya akimpatia tofari Kinana walipokuwa wakisaidia ujenzi wa Shule ya Msingi Unyaghumpi, katika Jimbo la Singida Mashariki la Mbunge Tundu Lissu. Mbunge huyo anadaiwa kuwakataza  wananchi kuchangia fedha za kujengea vyumba vya madarasa katika shule hiyo. Lakini baada ya kuona watoto wao wanateseka kwa kukosa elimu wananchi wameamua kupuuza katazo hilo na kuanza kujitolea kujenga vyumba hivyo vya madarasa.
ujenzi wa Shule ya Msingi Unyaghumpi ukiendelea katika Jimbo la Singida Mashariki la Mbunge Tundu Lissu,ambaye anadaiwa kuwakataza  wananchi kuchangia fedha za kujengea vyumba vya madarasa katika shule hiyo.imeelezwa na Wananchi wa jimbo hilo kuwa kufuatia na hali hiyo miradi mingi imekwama kwa miaka minne sasa,jambo ambalo limewarudisha nyuma kimaendeleo.
Jengo la Zahanati ya Kimbwi, Kata ya Mungaa, ambayo ilikamilika wakati Kata hiyo ikiongozwa na Diwani wa CCM, lakini hadi sasa haitumiki baada ya Diwani wa sasa wa Chedema na Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki, Tundu Lissu kudaiwa kuwakataza wananchi kuchangia fedha za ujenzi wa nyumba ya madaktari.
Kinana akizungumza na baadhi ya wananchi nje ya engo la Zahanati ya Kimbwi, Kata ya Mungaa, ambayo ilikamilika wakati Kata hiyo ikiongozwa na Diwani wa CCM, lakini hadi sasa haitumiki baada ya Diwani wa sasa wa Chedema na Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki, Tundu Lissu kudaiwa kuwakataza wananchi kuchangia fedha za ujenzi wa nyumba ya madaktari.
PICHA NA MICHUZIJR-IKUNGI SINGIDA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 22, 2014

    HIZO NI MBIO ZA KUTAFUTA NAFASI YA KUGOMBEA URAIS KAZI KWELI KWELI

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 22, 2014

    Michuzi wewe si fisadi tajiri katoe pesa ikamilishe ujenzi

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...