Wanafunzi
wa elimu ya awali, wakifundishwa na mwalimu Juliana Joseph huku wakiwa
wamekaa sakafuni na juu ya paa kukiwa wazi katika moja ya vyumba vya
madarasa ya Shule ya Msingi, Unyaghumpi vilivyozuiliwa kujengwa na
Mbunge Tundu Lissu kwa kuwakataza wananchi kuchangia fedha na kuwaambia
kuwa fedha zote zitatoka serikalini,imeelezwa na Wananchi wa jimbo hilo kuwa kufuatia na hali hiyo miradi mingi imekwama kwa miaka minne sasa,jambo ambalo limewarudisha nyuma kimaendeleo.
Katibu
Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akisaidia kuvuna mtama na uwele kwenye
shamba bibi mjane asiye na mtoto, Mayasa Mkhandi katika Kata ya
Unyaghumpi, Jimbo la Singida Mashariki, mkoani Singida,wakati wa ziara
yake ya kuimarisha uhai wa chama, kukagua, kuhimiza na kusukuma ujenzi
wa miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya
CCM, kukagua maandalizi ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na kusikiliza
kero za Wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.
Katika
Jimbo hilo linaloongozwa na Mbunge Tundu Lissu wa Chadema, Kinana
alishuhudia miradi mbalimbali ya maendeleo ambayo ujenzi wake
umekwamishwa na mbunge huyo kwa kuwzuia wananchi kuchangia fedha za
miradi hiyo akidai kuwa fedha zote zitatoka serikalini.
Baadhi
ya miradi iliyosimama aliyoikagua Kinana, ni Zahanati ya Kimbwi ukiwemo
ujenzi wa nyumba za waganga ambayo imeishia kwa kupigwa msingi wa zege.
Vyumba vya madarasa vya shule ya msingi Unyaghumpi ambapo walikutwa
watoto wa shule ya awali wakifundishwa huku wakiwa wamekaa sakafuni na
juu kukiwa wazi bila kuzekwa. Miradi mingine iliyokwama ni ujenzi wa barabara, mawasiliano ya simu, maji na umeme.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia katika mkutano wa hadhara ulofanyika katika Kijiji cha Makiungu, wilayani Ikingu, Jimbo la Singida Mashariki la Mbunge Tundu Lissu wa Chadema. Kinana alimponda Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki kwa kitendo chake cha kuwakataza wananchi kuchangia fedha za miradi maendeleo na kusababisha jimbo hilo kudorora kimaendeleo tofauti ma majimbo mengine nchini. Alisema badala ya kuwasaidia wananchi badala yake anaendekeza masuala ya UKAWA na kutukana matusi bungeni.
Katibu
Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia katika mkutano wa hadhara
ulofanyika katika Kijiji cha Makiungu, wilayani Ikingu, Jimbo la
Singida Mashariki la Mbunge Tundu Lissu wa Chadema. Kinana alimponda
Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki kwa kitendo chake cha kuwakataza
wananchi kuchangia fedha za miradi maendeleo na kusababisha jimbo hilo
kudorora kimaendeleo tofauti ma majimbo mengine nchini. Alisema badala
ya kuwasaidia wananchi badala yake anaendekeza masuala UKAWA na kutukana
matuzi bungeni.
Aliyekuwa kiongozi wa Chadema, Ismail Gwau, akitupilia mbali bendera ya CHADEMA mara baada ya kutangaza kujiunga na chama cha CCM,katika Mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye stendi ya mabasi mjini Ikungi.
Sehemu ya Wakazi wa Ikungi wakishangilia jambo kwenye mkutano wa hadhara.
Mmoja
wa Viongozi wa CCM,Wilaya akimpatia tofari Kinana walipokuwa wakisaidia
ujenzi wa Shule ya Msingi Unyaghumpi, katika Jimbo la Singida Mashariki
la Mbunge Tundu Lissu. Mbunge huyo anadaiwa kuwakataza wananchi
kuchangia fedha za kujengea vyumba vya madarasa katika shule hiyo.
Lakini baada ya kuona watoto wao wanateseka kwa kukosa elimu wananchi
wameamua kupuuza katazo hilo na kuanza kujitolea kujenga vyumba hivyo
vya madarasa.
ujenzi wa Shule ya Msingi Unyaghumpi ukiendelea katika Jimbo la Singida Mashariki la Mbunge Tundu Lissu,ambaye anadaiwa kuwakataza wananchi kuchangia fedha za kujengea vyumba vya madarasa katika shule hiyo.imeelezwa na Wananchi wa jimbo hilo kuwa kufuatia na hali hiyo miradi mingi imekwama kwa miaka minne sasa,jambo ambalo limewarudisha nyuma kimaendeleo.
Jengo
la Zahanati ya Kimbwi, Kata ya Mungaa, ambayo ilikamilika wakati Kata
hiyo ikiongozwa na Diwani wa CCM, lakini hadi sasa haitumiki baada ya
Diwani wa sasa wa Chedema na Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki, Tundu
Lissu kudaiwa kuwakataza wananchi kuchangia fedha za ujenzi wa nyumba
ya madaktari.
Kinana akizungumza na baadhi ya wananchi nje ya engo
la Zahanati ya Kimbwi, Kata ya Mungaa, ambayo ilikamilika wakati Kata
hiyo ikiongozwa na Diwani wa CCM, lakini hadi sasa haitumiki baada ya
Diwani wa sasa wa Chedema na Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki, Tundu
Lissu kudaiwa kuwakataza wananchi kuchangia fedha za ujenzi wa nyumba ya
madaktari.
PICHA NA MICHUZIJR-IKUNGI SINGIDA
HIZO NI MBIO ZA KUTAFUTA NAFASI YA KUGOMBEA URAIS KAZI KWELI KWELI
ReplyDeleteMichuzi wewe si fisadi tajiri katoe pesa ikamilishe ujenzi
ReplyDelete