Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais (Kazi Maalum) Profesa Mark Mwandosya (wa tatu kushoto) akimsikiliza kwa makini Meneja Mkuu wa Benki ya CRDB tawi la Burundi,Bruce Mwile (kulia) wakati alipotembelea Makao Makuu ya CRDB yaliopo mjini Bujumbura,nchini Burundi.Wengine pichani toka kushoto ni Bi. Muna Mahanyu,Mkurugenzi wa Sheria EWURA,na Ndugu Elias Tamba,Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Burundi.
Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais (Kazi Maalum),Prof. Mark Mwandosya (wa nne kushoto) na Bw.Bruce Mwile,Meneja Mkuu wa CRDB Burundi (wa nne kulia),wakiwa mbele ya jengo la Makao Makuu ya CRDB Burundi ambapo pia lipo tawi la benki hiyo la Inyereri lililofunguliwa mwaka mmoja na nusu uliopita.Wengine katika picha kutoka kushoto ni Nd. Makiri Ngangaji,kutoka SUMATRA,Nd. Ngusa Izengo,Katibu wa Waziri wa Nchi,Nd.Elias Tamba,KaimuBalozi, Bi.Miriam Mahanyu,kutoka EWURA,Nd.Massawe Antony,kutoka DAWASA na Nd.Almasle Burundi,Afisa wa Itifaki.
Tawi la tatu la CRDB Burundi alilotembelea Waziri Mark Mwandosya,wa tatu kushoto, ni lile la Asiatique.
Hapa Waziri yuko pamoja na Bruce Mwile, wa tatu kulia, na ujumbe wake. 
Waziri Mwandosya ameipongeza Benki ya CRDB Burundi kwa maendeleo makubwa kwa kuongeza mtaji wake zaidi ya mara tatu katika kipindi kifupi sana tangu kuanzishwa kwake nchini Burundi.Wazri Mwandosya ameipongeza CRDB kwa kuwa Benki ya kwanza ya kitanzania kuanzisha biashara nje ya nchi.Amesema CRDB imekuwa na dira na dhima thabiti iliyoiwezesha kufanya hivyo.CRDB imethubutu kuwekeza nje ya nchi,na imewezekana.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 22, 2014

    Hongereni sana CRDB. KEEP IT UP

    ReplyDelete
  2. Congratulations Mr. Mwile and CRDB. Go, go CRDB, go meet the South African banksbin the African plains!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...