*Ataka viongozi wa dini wasichoke kuombea amani ya Taifa 

 WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amesema Serikali itaendelea kusimamia msimamo wake wa kutokuwa na dini wala nchi kutokuwa na dini lakini itaendelea kuruhusu watu wawe na dini zao. 
 Ametoa kauli hiyo leo mchana (Jumapili, Mei 25, 2014) kwenye ibada ya kumuweka wakfu Askofu Mteule Conrad Nguvumali wa Kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la Rukwa iliyofanyika kwenye Uwanja wa Nelson Mandela, mjini Sumbawanga. 
 Waziri Mkuu ambaye alikuwa mgeni rasmi kwa niaba ya Rais Jakaya Kikwete ambaye yuko nje ya nchi kikazi, alisema: 
“Leo tukiruhusu Serikali iwe na dini na tayari katika dini zote kuna makundi madogo madogo, je wale wa upande mwingine utawaacha wapi?”. 
 Pia alitumia fursa hiyo kuwaasa viongozi wa dini nao pia waangalie wasitumbikie kwenye mtego wa siasa na kuruhusu kanisa zima liwe la chama fulani kwani miongoni mwa waumini wao wapo pia wapenzi wa vyama vingine. 
 “Kama mtu binafsi, kiongozi wa dini anaweza kuwa mpenzi wa chama lakini kama Kanisa tusiruhu hali hiyo,” alionya. Aliwaomba viongozi wa dini waendelee kuliombea Taifa na hasa waombee amani ya Taifa hili. 
“Ninawasishi viongozi wa dini msichoke kuombea amani ya Taifa hili kwani amani ikipotea kama nchi hatuna mahali pa kukimbilia.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akimpongeza Askofu Conrad Ernest Nguvumali baada ya kuwekwa Wakfu kuwa Askofu wa Kanisa la Moravian jimbo la Rukwa katika ibada iliyofanyika kwenye uwanja wa Nelson Mandela mjini Sumbawanga May 25, 2014.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akimkabidhi zawadi ya picha Askofu wa Kanisa la Moraviani jimbo la Rukwa, Conrad Ernest katika ibada ya kumwapisha askofu huyo iliyofanyika kwenye uwanja wa Nelson Mandela mjini Sumbawanga May 25,2014.. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...