![]() |
Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mhe. Ernest Ndikilo akiongea na wanahabari |
Mkuu
wa Mkoa wa Mwaza anapenda kuwafahamisha ya kwamba, siku ya madhimisho ya
mazingira Duniani, hufanyika kuanzia tarehe 01 hadi 05 ya mwezi Juni, kwa kila Mwaka. Kwa
mwaka 2014 shirika la Umoja wa mataifa linalo shughulikia mazingira limetangaza
Kaulimbiu ya maadhimisho hayo kuwa ni “RAISE YOUR VOICE BUT NOT THE SEAL LEVEL” kwa tafsiri ni “CHUKUA HATUA KUKABILIANA NA TABIANCHI na
kitaifa” TUNZA MAZINGIRA ILI KUKABILIANA NA MBADILIKO YA TABIANCHI.
Kwa
mwaka huu wa 2014 Mkoa wetu wa Mwanza umeteuliwa
kuwa mwenyeji wa kitaifa, kwa wiki ya
maadhimisho ya Mazingira Duniani, ambapo katika juma hilo shughuli mbalimbali
zitafanyika ikiwa ni pamoja na kufanya usafi katika maeneo mbalimbali,
kuhamasisha wananchi kuhusu utunzaji wa Mazingira kwa njia ya Makongamano, kupanda miti, kuzoa
takataka, maonesho ya utunzaji na mazingira, kuondoa magugu katika Ziwa
Victoria na ufugaji wa nyuki pamoja na kufanya ziara kwenye maeneo tofauti
yanayo jishughulisha na utunzaji wa mazingira ikiwemo viwanda.
Ufungunguzi
wa maadhimisho kitaifa utafanyika tarehe 02 Juni, 2014 kuanzia saa 1.00 asubuhi
katika Viwanja vya Furahisha na siku ya kilele itakuwa tarehe 05 Juni,
2014 ambapo Mgeni rasmi atakuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Dkt. Mohamed Gharib Bilal.
Shughuli
zitakazo fanyika siku hiyo ni pamoja na-; kukabidhi vyeti kwa wadau mbali mbali
wa mazingira, zawadi na tuzo za utunzaji uhifadhi wa mazingira pamoja na zawadi
kwa washindi wa wa kuhifadhi mazingira.
Aidha Mkoa unategemea kupokea Wageni wa Kitaifa na Kimataifa, Aidha Viongozi wa Kitaifa
watatembelea Makampuni na kuona utunzaji wa Mazingira na jinsi ya kutenga taka
ngumu na zisizo ngumu.
Nichukue
fursa hii kutoa rai kwenu kuwa “ ukitaka kuona mgeni anafurahia makaribisho
yako ukarimu ni kitu muhimu sana, Nawaomba wananchi wajitokeze kwa wingi na
kuwalaki wageni wote watakao tufikia katika juma zima hilo lakini pia kama
ilivyo desturi yetu wanamwanza tuonyeshe ukarimu kwa wageni wetu na pindi
waondokapo basi waikumbuke Mwanza.
“TUNZA MAZINGIRA, KUKABILIANA NA MABADILIKO
YA TABIANCHI”
IMETOLEWA
NA MKUU
WA MKOA WA MWANZA.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...