Msanii wa Bongo Movie, Rachel Haule ‘Recho’ (pichani chini), amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es slaaam. 
Baadhi ya wasanii wa Bongo Movies wakiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili baada ya taarifa za msiba wa msanii mwenzao, Rachel Haule 'Recho' mapema leo.
Habari zilizothibitishwa na Mwenyekiti wa Bongo Movie, Steve Nyerere, zimesema kuwa Recho alikwenda Muhimbili jana kujifungua ambapo mara baada ya kujifungua mtoto alifariki.
Yeye mzazi pia hali yake iligeuka na kuwa mbaya, na ikabidi  ahamishiwe ICU ambako hali ilizidi kuzorota na baadae kufariki dunia. 
Globu ya Jamii inatoa mkono wa rambirambi kwa ndugu, jamaa na marafiki na wadau wote wa tasnia ya filamu kwa msiba huu mzito

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 28, 2014

    Ya hapa duaniani ndio mwisho wake. Sasa anajua yeye alilolitenda duniani na lililobaki ni kwenda kuangalia maisha ya Akhera jee alifanya kwa ajili ya Muumba au alifanya kwa matakwa ya roho na akili yake. Jibu analo yeye hapo atakapokutana na Mola muumba wa kila kilichopo duniani hapa

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...