Na Sylvester Onesmo 
wa Jeshi la Polisi Dodoma. 
 Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Jackson s/o Venance, umri miaka 33, kabila Mhaya, mfanyakazi wa NSSF Bukoba aliyekuwa akitembea kwa miguu pembeni mwa barabara ya Nyerere maeneo ya TRA Dodoma katika Manispaa na Mkoa wa Dodoma amefariki dunia alipokuwa akitibiwa katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma baada ya kugongwa na gari lenye namba za usajili T.399 CWG aina ya NISSAN iliyokuwa ikiendeshwa na Dotto d/o Onesmo, umri miaka 25, kabila msukuma, mwanafunzi wa Chuo cha Mipango Dodoma. 
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi David Misime – SACP amesema kabla ya kifo chake, Marehemu alifika Dodoma kwa ajijli ya kuchukua cheti chake katika Chuo cha Biashara Dodoma (CBE). 
 Kamanda Misime amesema uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa chanzo cha ajiali hiyo ni uzembe wa dereva wa gari kutokuwa mwangalifu. 
Uchunguzi zaidi wa ajali hiyo unaendelea na dereva atafikishwa mahakamani muda wowote kuanzia jumatatu mara baada ya taratibu kukamilika. 
 Aidha Kamanda Misime ametoa wito kwa madereva wa Magari na Pikipiki (Bodaboda) kuwa wawe na udereva wenye tahadhari ambao utaweza kupunguza ajali zisizo za lazima. 
Pia amewataka madereva hao wakumbuke kuwa wanapoendesha maeneo ya makazi na mikusanyiko ya watu wazingatie mwendo wao usizidi na uwe chini ya speed 50 zilizotamkwa kisheria. 
 Alisisitiza kuwa atakaye kiuka maelekezo hayo ya kisheria atachukuliwa hatua kali za kisheria.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...