Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (kulia) akizungumza na Naibu Balozi
wa Uingereza nchini Tanzania, Penny Smith (katikati) masuala mbalimbali ya ushirikiano kati
ya nchi yake na Tanzania. Kushoto ni Mshauri wa Haki Jinai, Ubalozi wa Uingerzea nchini,
Lindsey McNally. Mazungumzo hayo yalifanyika katika ofisi ya Waziri Chikawe, Barabara ya
Ohio, jijini Dar es Salaam leo.
Mshauri wa Haki Jinai, Ubalozi wa Uingereza nchini, Lindsey McNally (kushoto) akimfafanulia
jambo Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (kulia) kuhusiana na masuala
mbalimbali ya ushirikiano kati ya nchi yake na Tanzania. Katikati ni Naibu Balozi wa Uingereza
nchini, Penny Smith. Mazungumzo hayo yalifanyika katika ofisi ya Waziri Chikawe, Barabara
ya Ohio, jijini Dar es Salaam leo.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (wapili kushoto), Naibu Balozi wa
Uingereza nchini, Penny Smith (wapili kulia), Mshauri wa Haki Jinai, Ubalozi wa Uingereza
nchini, Lindsey McNally (kushoto) na Kamishna wa Pasipoti na Uraia, wa Idara ya Uhamiaji,
Victoria Lembeli wakiwa katika picha ya pamoja baada ya mazungumzo marefu yaliyofanyika
katika ofisi ya Waziri Chikawe, Barabara ya Ohio, jijini Dar es Salaam leo. Picha na Felix
Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
mi miguu ya Mshauri Haki Jinai...sijuui peponi pakoje, kama hapa Duniani watu "wamejaaliwa" namna hiyo.
ReplyDeleteHicho kiguo cha Mshauri unachokisema ni kutoheshimu tamaduni za watu tu na viongozi wao! Mbona Naibu Balozi kavaa heshma? Unadhani angevaa hivo Uarabuni?
ReplyDeletekaka hapo juu umenena du! miguu si mchezo. ukaaji gani lakini huu jamani. waziri kazi aliipata
ReplyDelete"...sijuui peponi pakoje, kama hapa Duniani watu "wamejaaliwa" namna hiyo."
ReplyDeleteNani kakwambia kuna mahali panaitwa peponi?