MIMI MARIDADI KILONZO KUTOKA MUHEZA, TANGA, TANZANIA NAMTAFUTA NDUGU YANGU  ALIYEKUWA ANAITWA MWANAHAWA KILONZO, AMEZALIWA MWAKA 1986 (06 NOVEMBA) NA AKABADILISHA JINA NA KUITWA ROSE MICHAEL GAVIGAN WAKATI ALIPOCHUKULIWA NA SHANGAZI YETU REHEMA NGAMI (KILONZO MDHAM) NA MUME WAKE MICHAEL GAVIGAN KWENDA KUISHI NAYE UINGEREZA MWAKA 1993. 

TANGU MWAKA HUO HAJARUDI TENA NA HATUNA MAWASILIANO NAYE TENA. SHANGAZI REHEMA ALISHARUDI TANGU MWAKA 1997 NA BAHATI MBAYA AMEFARIKI MWEZI APRIL 2014. 

MAMA NAYE ALISHAFARIKI SIKU NYINGI. KABLA SHANGAZI HAJAFARIKI ALITUACHIA ANUANI HIZI ZIFUATAZO AMBAZO HATUNA UHAKIKA KAMA WAHUSIKA BADO WAKO HAPO KWANI TULIANDIKA BARUA LAKINI HATUJAPATA MAJIBU:- 

MICHAEL GAVIGAN, MRS. R. GAVIGAN,
69 THORNEYWOOD RISE, 10 FREDERICK AVE
THORNEYWOOD, CARLTON,
NOTTINGHAM, NOTTINGHAM,
NG 3 2PE, NG4, IHP,
ENGLAND. ENGLAND. 

KWA HIYO HAKUNA MTU ANAYEFAHAMU HABARI ZAKE TENA. MARA APATAPO UJUMBE HUU TAFADHALI NAOMBA AWASILIANE NAMI KWA NAMBA +255656487459.

HAPA NAAMBATANISHA PICHA ZA ROSE (MWANAHAWA) NILIZOFANIKIWA KUZIPATA.
NASHUKURU SANA.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 05, 2014

    Tupo Nottingham tutajitahidi kumtafuta Kwenye anuani Hilo

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 05, 2014

    Tumia page hii kumtafuta wengi waliwapata ndugu zao ila inahitaji kuregister fifteen pounds kwa kuanzia
    http://www.ancestry.co.uk/?o_iid=41012&o_lid=41012&o_sch=Web+Property

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 05, 2014

    na huku London tutaulizia pia, Maisha haya

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 06, 2014

    Ukienda kwenye hii site
    http://lincolnshire.ukwhite.net/gavigan-michael-1832936.html
    Utaona kuwa huyu ndugu bado anaishi hii address iliyotumwa. Kwa waliopo huko jaribuni hii namba: 115.950046


    Gavigan Michael

    Thorneywood Rise 69 #H
    Nottingham
    NG32PE
    Telephone: 115.950046
    eMail:

    Record Last Updated: March 6th, 2014

    Read Our Disclaimer

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 06, 2014

    Nashukuru sana kwa maoni yenu. Naomba kufanya marekebisho kidogo kuhusu hizo picha. Picha ya Mama mtu mzima mwenye nguo ya pink ni shangazi yetu Rehema aliyefariki na hiyo nyingine ya mtoto mwenye gauni jekundu na mzungu ndiyo ya huyo anayetafutwa (mtoto Mwanahawa au Rose). Nawashukuru sana kwa msaada wenu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...