Mkuu wa Wilaya ya Bahi Mkoani Dodoma Betty Mkwassa (wa ttau kushoto) akipokea moja ya vitanda 9 kutoka kwa Mkuu wa Vodacom Kanda ya Kati Mruta Hamisi vilivyotolewa na mfuko wa kampuni hiyo wa kusaidia jamii (Vodacom Foundation) kwa ajili ya wodi ya wanawake katika kituo cha afya cha kijiji cha Chipanga.Kampuni ya Vodacom imejikita katika kusaidia uboreshaji wa huduma za afya hasa kwa wanawake na watoto chini ya mpango wake wa uwajibikaji kwa jamii.
Mama mjamzito Vailet Petro (katikati) mkazi wa kijiji cha Chipanga, Wilaya ya Bahi Dodoma akimwaga chozi la furaha mbele ya Mkuu wa Wilaya hiyo Betty Mkwassa (kushoto) na Mkuu wa Vodacom Kanda ya Kati (kulia) baada ya kushuhudia kituo cha afya cha kijini hapo kikipokea vitanda tisa kutoka Vodacom Foundation kwa ajili ya wodi ya wanawake. . Msaada huo umewaondolea adha akina mama ambao walikuwa wakilala sakafuni kutokana na uhaba mkubwa wa vitanda uliokuwa ukikikabili kituo hicho.
Baadhi ya Wananchi wa kijiji cha Chipanga wakisaidia kubeba vitanda vya msaada vilivyotolewa na Vodacom Foundation kuvipeleka katika wodi ya akinamama tayari kwa ajili ya matumizi.Vitanda hivyo vilikuwa na thamani ya Sh 10 Milioni .
Mkuu wa Wilaya ya Bahi Betty Mkwassa (katikati) akiteta na Mkuu wa Vodacom kanda ya kati Mruta Hamisi wakati walipokuwa wakimjulia hali mzazi aliyejifungua katika kituo cha afya Cha Chipanga wilayani Bahi.Kituo hicho huhudumia wakazi wa Bahi mka wa Dodoma na Manyoni mkoani Singida. Vodacom Foundation imekabidhi vitanda 9 vya wagojwa kwa ajili ya wodi ya wanawake yenye uhaba mkubwa wa vitanda.
Mkuu wa Wilaya ya Bahi, Mkoani Dodoma Betty Mkwasa, akiongea na Wananchi wa kijiji cha Chipanga kabla ya kupokea msaada wa vitanda kwa ajili ya zahanai ya kijijini hapo vilivyotolewa na Vodacom Foundation kuboresha huduma za afya kwa mama na mtoto.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...