Pichani kati Mgeni rasmi,Mh.William Ngelleja akizindua albamu mpya ya nyimbo za injili ya muimbaji Grace Mwikwabe (pichani shoto) na kulia ni Mkurugrenzi wa Msama Promotions ambao ndio waandaji wa matamasha hayo ya pasaka na Xmass.
Mgeni rasmi katika muendelezo wa tamasha la Pasaka,ambaye ni Mbunge wa jimbo la Sengerema,Mh.William Ngereja akizungumza machache mbele ya umati mkubwa wa wakazi wa jiji la Mwanza waliojitokeza kwenye tamasha hilo,Ngeleja aliwataka viongozi mbalimbali kuliombea Taifa wakati likipita katika kipindi hiki kigumu cha mchakato wa kuipata Katiba mpya, na pia aliwataka Wananchi nchini Kote kuwa watulivu,kwani Mungu ni mwema mchakato wa kuipta katiba mpya utakwisha tu na katiba itapatikana.
Mkurugenzi wa Msama Promotions,Alex Msama akitoa neno la Shukurani kwa viongozi wa dini mbalimbali pamoja na wakazi wa jiji hilo waliojitokeza kwa wingi kwenye tamasha la mwendelezo wa Pasaka,lililofanyika ndani ya uwanja wa CCM Kirumba hapo jana,Wakati huo huo katika tamasha hilo mgeni rasmi alikuwa ni Mh.William Ngeleja.
Rebecca Malope akiimba kwa hisia jukwaani.
Mwimbaji
nyota wa injili hapa nchini Rose Muhando akiwaimbisha washabiki na
wapenzi wa nyimbo za injili wimbo wake mpya wa facebook na twitter ndani ya uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza
hapo jana wakati wa mwendelezo wa tamasha la pasaka,ambalo limepokelewa
vyema na wakazi wa jiji hilo.
Mambo ya Facebook,Twitter na Instargram hayo live
Mwimbaji nyota wa nyimbo za kiroho kutoka nchini Afrika Kusini,Rebecca Malope akitumbuiza jana jion katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza,ikiwa ni sehemu ya mwendelezo wa tamasha la Pasaka huku likiwa limebeba kauli mbiu maridhawa kabisa isemayo Tanzania Kwanza,Haki Huinua Taifa.
Sehemu ya umatii wa watu wakifuatilia tamasha hilo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...