Na John Gagarini, Kibaha
CHAMA cha Msalaba Mwekundu mkoani Pwani kimesema kuwa kitaendela
kuisaidia jamii ambayo inauhitaji pamoja na wale wanaokumbwa na
majanga mbalimbali.
Hayo yamesemwa mjini Kibaha na katibu msaidizi wa chama hicho
Felisiana Mmasi wakati wakitoa misaada ya viatu na vifaa vya shule kwa
wanafunzi wa shule ya sekondari Nyumbu na vituo vya kulelea watoto
wanaoishi kwenye mazingira magumu vya THADEI na Buloma vilivyopo kata
ya Picha ya Ndege na Mkuza wilayani Kibaha.
Mmasi alisema kuwa lengo la chama hicho ni kuwasaidia watu wenye
matatizo mbalimbali kwenye jamii ikiwa ni pamoja na kutoa msaada
kwenye majanga na maafa yanoyojitokeza.
"Mbali ya kutoa viatu pia tumetoa madaftari na kalamu ambapo
tutaendelea kusaidia wanafunzi waishio kwenye mazingira magumu kwenye
mkoa mzima ambapo baadhi ya wilaya tayari zimeshapatiwa misaada hiyo,"
alisema Mmasi.
Kwa upande wake mratibu wa mradi wa Life kupitia chama hicho Kibaha
Mjini Agnes Lubogo alisema kuwa mbali ya kusaidia kutoa misaada
mbalimbali pia wanasaidia kuwahudumia wagonjwa wa UKIMWI walio
majumbani.
Lubogo alisema kuwa wanahudumia wagonjwa ambao watoro ambao hawapati
huduma mahospitalini hivyo kuwafuata huko waliko ambapo wana wahudumu
wa nyumbani wapatao 73.
OFISA WA RED CROSS PWANI ISARIA TOWO AKIWAPATIA MADAFTARI
WANAFUNZI WA KITUO CHA THADEI MADAFTARI KATIKA MAADHIMISHO YA SIKU YA CHAMA HICHO YALIYOFANYIKA MJINI KIBAHA PICHA NA JOHN GAGARINI
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...