Kamera ya Globu ya Jamii,mchana wa leo imepita kwenye barabara ya Morogoro rodi kuanzia Magomeni mpaka Shekilango na kukuta malundo ya taka ngumu yakiwa yamekusanywa kwa mafungu mafungu namna hii.hapo ndipo swali likanijia,kwamba hivi uhifadhi taka wa namna hii umeruhusiwa kisheria ama ni ndio mambo yetu yake yale kuleana.?? na kama ni Sheria ni ipi inayoruhusu uchafuzi wa mazingira namna hii?? nilijikuta nikikosa majibu na ndipo ilipobidi kuja na mada hii hapa Globu ya Jamii ili tuweze kusea aidia.picha hii imepigwa Magomeni Kagera.
 mbele kidogo ya kituo cha Magomeni Kagera kuna lundo lingine kama lionekanavyo pichani na nyuma ya taka hizo kuna mgahawa wa Mama ntilie ambaye anawauzia watu Chakula. 
Hili lingine liko Manzese karibu kabisa na Kituo cha kwa Bahresa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 05, 2014

    Dar pazuri!!

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 05, 2014

    ndugu michuzi asante kwa kuleta mada hii , mimi binafsi naweza sema kosa ni la serikali ya mitaa na wanaopewa tenda za kuzoa taka, kwa sababu wao ndo wanawaambia wananchi wakusanye hapo barabarani ili wakija na gari lao wasipate tabu kuingia mitaani , mimi binafsi mtaa wangu naoishi kkoo tumeambiwa wote tuwe tunakusanya taka nje kwa kuwa magari ya taka yanapita usiku wa manane na kuzoa , sasa tatizo linakuja kama gari halikupita siku moja basi inakuwa kero ya harufu siku yote ile , mimi nilishangaa kwa kufanya utaratibu wa wao kuzoa taka usiku wakati watu wakiwa wamelala nikauona kama sio mzuri , kwani mkandarasi aliyepewa tenda ya kuzoa taka kabla ya huyu wa sasa yeye alikuwa akizoa asubuhi na mchana , sasa huyu wa sasa anazoa usiku, nikaambia asubuhi wanasababisha foleni ,nikawa sina la kusema ... sasa ushauri wangu kwa wahusika kuwa na vyombo vyao wanaweka vikubwa au hata matera wananchi wanayajaza wao wakija wanayavuta tena yawe na mifuniko , kama pale mjini kitumbini karibu na petrol steshen nimeona wameweka , sasa inakuwaje waweke baadhi ya sehemu tu ? au hawa wa huku hawastahili mazingira safi ? asante na wawajibishwe

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 05, 2014

    Ni nchi gani hii???? ni swali tu!

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 06, 2014

    SHERIA HII INAITWA " KILA KITU CHAWEZEKANA BONGO ONLY".

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 06, 2014

    Hapa bongo bana, unataka sheria ya nini? Kama na wewe unahamu ya kutupa taka barabarani tupa hakuna shida.

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 06, 2014

    Uchafu unatisha.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...