Mhe. Naimi Aziz, Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia na mwakilishi wa kudumu katika Umoja wa Afrika akiongoza mkutano wa Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika uliofanyika tarehe 2 Mei 2014 mjini Addis Ababa, Makao Makuu ya Umoja huo. Tanzania itakuwa mwenyekiti wa chombo hicho muhimu kinachoshughulikia Amani na Usalama barani Afrika kwa kipindi cha Mwezi Mei 2014. Katika kipindi cha Uwenyekiti wake, Tanzania pamoja na mambo mengine itaongoza Baraza hilo katika kujadili na kutafuta ufumbuzi wa kudumu wa migogoro inayoendelea huko mashariki ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Sudani ya Kusini,, Afrika ya Kati, Mali na ukanda wa Sahel, pamoja na Darfur, Sudan. Aidha, Tanzania itaongoza mjadala wa wazi (open session) kuhusu hali ya watoto katika migogoro barani Afrika ( Children in Armed Conflicts in Africa). Tanzania itaongoza pia mkutano wa pamoja wa majadiliano ( joint consultative meeting) kati ya Baraza la Amani na Usalama la Afrika na Baraza la Amani na Usalama la Ulaya utakaofanyika Brussels, Ubelgiji. Wakati wa kusherehekea miaka 10 ya kuanzishwa kwa Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika tarehe 25 Mei 2014, Tanzania itaongoza mjadala kuhusu "Miaka 10 ya Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika mafanikio, changamoto zilizopo na namna ya kusonga mbele".
Bw. Samwel Shelukindo, Afisa Mambo ya Nje Mkuu wa Ubalozi wa Tanzania Addis Ababa akiwa katika kikao cha Baraza la Amani na Usalama la Afrika kilichokuwa kinaongozwa na Mhe. Balozi Naimi Aziz wa Tanzania.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...