Marehemu Lilian Peppi Gondwe.

UONGOZI wa Azania Benki unatangaza kifo cha Mfanyakazi wake,Lilian Peppi Gondwe kilichotokea  usiku wa kuamkia leo Jumatatu Mei 5 katika hosptali ya Arusha Medical Center ya jijini Arusha  alipokuwa akipatiwa matibabu ya Saratani.

Mipango ya Mazishi inafanyika  nyumbani kwa marehemu eneo la Kimandolu jijini Arusha ambapo mazishi yanatarajia kufanyika Alhamis Mei 8 mwaka huu katika makaburi ya Njiro baada ya sala itakayofanyika katika kanisa la kiinjili la kilutheli (KKKT)Kimandolu .
Tulikupenda Lilli , lakini MUNGU amekupenda zaidi... tangulia, mbele yako nyuma yetu. Mungu akupe makazi mema PEPONI, Ameen.
Imetolewa na uongozi wa Azania uongozi wa Azania Benki.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 05, 2014

    Poleni sana wafiwa. jamani naomba msaada wenu huyu Lilian Gondwe ndo yule ninayemfahamu Mimi?. Alikuwa anaishi Mwanza akasoma Nyanza Primary School? ndo huyu aliyekuwa EXIM BANK? Mimi nimesoma naye Mwanza Nyanza kama ndo yeye jamani msiba huu umenigusa sana na alikuwa best friend wa sister yangu kama ni yeye. HAKIKA BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA na wote tumetoka kwake na huko huko tutarejea.

    ReplyDelete
    Replies
    1. AnonymousMay 05, 2014

      Huyu dada ni alikuwa mzuri I saw her once Exim bank Enzi hizo I think ni dada wa Jemima Gondwe

      Delete
    2. AnonymousMay 05, 2014

      Ndio Huyo Huyo Alisoma nyakahoja

      Delete
    3. AnonymousMay 05, 2014

      Ndio huyohuyo mdada alikuwa mzurije .Dah ehh baba mpumzishe lilian .Baba ao alikuwaga mzambia manager wa mwatex.

      Delete
  2. AnonymousMay 05, 2014

    "REQUIESCAT IN PACE" LILIAN!

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 05, 2014

    Ooh no jamani hatukuwasiliana miaka mingi sana. Pumzika kwa amani mwenyezi mungu akulaze mahali pema. Amina

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 05, 2014

    Poleni jemima gondwe nakumbuka alikuwaga anakujaga kukuona tambaza

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 06, 2014

    R.I.P Lilian hakika Umetangulia nasi wote tuko njia moja kwani hatujui saa wala dakika. Kama kuna viumbe waliumbika basi Lilian ilikuwa mmoja wao na hakika jana nimeshtuka sana baada ya kuona tangazo hili. Lilian ulikuwa mzuri na cha zaidi ulijiheshimu sana. Nakumbuka sana enzi zile ulivyokuwa unasoma pale Nyanza PS na jinsi nilivyokuwa nakupenda na ingawa nilikuwa mdogo sana ila niligundua uzuri wako wa kweli. Kapumzike kwa AMANI Lilian kweli Duniani tunapita, sisahau jinsi nilivyokuwa najificha mahala kule BUNGANDO ili nione unapita ukirudi kwenu hakika MOLA AMEUMBA na AMEAMUA KUCHUKUA KIUMBE CHAKE. Lilian ulikuwa na tabia ya pekee haswa upole na kujiheshimu nakumbuka mwaka 1988 or 1989 ndo ilikuwa mara ya mwisho kukuona tena nilikuona kwa mbali sikubahatika kukusemesha. Wafiwa wote poleni sana na jua hamko peke yenu tuko pamoja kwenye kuombeleza. PUMZIKA KWA AMANI LILIAN

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 06, 2014

    Huyu dada alikuwa mzuri EEh mungu baba apumzike kwa Amani .yaani kidogo nipigwe bunduki na Mzee gondwe .Dada ulikuwa mzuri wewe astakafulai Dah nilienda kusoma IFM ili tu nikupate vikashindikana .Natamani Mungu anichukue nikufuate mpaka mbinguni aisee.Rip lilian mungu amekuchukua na akupumzishe salama

    ReplyDelete
  7. mimi pia mdahu wa ulaya nimeshutushwa sana na kifo cha lilian nakumbuka mara ya mwisho kumuona ilikuwa posta yapata miaka tisa poleni sana napia niliwahi soma nae nyanza pl henzi hizo

    ReplyDelete
    Replies
    1. AnonymousMay 07, 2014

      Alikuwa mzuriiii .mguuu huo ,macho ,kiuno,rangi ya mwili,mtoto mwendo wa madaha ,ulitulia .RIP lili

      Delete
    2. AnonymousMay 07, 2014

      Watoto wa Mzee gondwe kwa kutulia kujificha .Huyu lili amefariki may 5 2014 .Nyie wote mlio comment Mara ya mwisho kumuona Mara 1989 Mara miaka 9 imepita .Mdogo wake nae adimu Huyo ukimuona Leo hutomwona mpaka sijui lini .RIP lilian

      Delete
  8. AnonymousMay 09, 2014

    RIP LIilia! You was a striuggling woman!

    ReplyDelete
    Replies
    1. AnonymousMay 09, 2014

      Grounded,pretty,independent,self discipline .Yaani Mimi sijawahi mwanamke mzuri mnoo alietulia .Rest in peace mtoto mzuri lili nilikupenda mnooo ila sikubahatika

      Delete
  9. AnonymousMay 05, 2015

    Today is one year anniversary my sister I love you ,miss you

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...