 |
Sehemu ya foleni ya malori ikielekwa kubeba mzigo katika kiwanda cha Saruji cha Dangote kilichopo katika eneo la Obajana, Jimbo la Kogi, kilomita 400 Kaskazini Mashariki mwa mji maarufu wa kibiashara wa Nigeria, Lagos.
Kwa sasa Kiwanda hicho kinazalisha tani za kimetriki milioni 10.25 kwa mwaka na hivyo kukifanya kiwanda hicho kuwa kiwanda kikubwa zaidi cha saruji duniani kilichoko katika eneo moja.
Baada ya upanuzi unaoendelea kufanywa kwenye kiwanda hicho, uwezo wake wa uzalishaji utaongezeka na kufikia tani za kimetriki 13.0 kwa mwaka. Kiwanda hicho kilicho kwenye eneo la kilomita za mraba saba kitakuwa kimegharimu kiasi cha dola za Marekani bilioni 2.5 wakati upanuzi wake utakapokamilika mwakani. Kwa sasa kiwanda hicho kina biashara ya dola za Marekani bilioni mbili kwa mwaka.
Kiwanda hiki , kilichoanza kujengwa mwaka 2003 na kukamilishwa mwaka 2006, na hatimaye awamu zake za kwanza na za pili kuzinduliwa rasmi na Rais Olusegun Obasanjo Mei 12, mwaka 2007, wiki mbili kabla ya kustaafu Urais wa Nigeria, kinaajiri watu 800 kwa wakati mmoja na hivyo kuwa miongoni mwa waajiri wakubwa zaidi katika Nigeria. |

Sehemu ya malori yakiwa katika foleni ya kusubiri zamu kuelekea kiwandani kupakia mzigo
Malori zaidi
Uwanja wa ndege binafsi wa kiwanda cha saruji cha Dangote.
Asante kwa "Mapicha ya kumwaga".Vipi Blog ya jamii ilijaribu kupata BEI ya mfuko mmoja wa simenti unagharimu kiasi gani(kwenye dola za kimarekani) nchini Naijeria(Nigeria)??Kwa Tanzania mfuko mmoja wa Simenti unagharimu karibu dola za kimarekani 9.1(kadirio la kiwango cha ubadilishaji fedha=Sh.1645 kwa dola 1 ya Kimarekani) au zaidi,hii ni kwa Daresalaam hadi huko mikoani.Nataka kulinganisha bei tu,nachelea kusema bei ya Simenti Tanzania iko juu sana.Na kila Mtanzania aliyeko nje ya nchi anaweza kutupatia "local price/bag" ya Simenti alipo tulinganishe.Mwisho
ReplyDeleteDavid V
alhajj usipoipata pepo ya Mungu itabidi tu ujilaumu
ReplyDeletemi nadhani baba mkwe angemwomba jamaa aje hata >Bagamoyo, manake sehemu za msata kulingana na utafiti kuna malighafi cement nzuri ya kiwango kama cha wazo Hill
ReplyDeleteMdau Anonymous hapo juu huyu jamaa tayari yupo bongo anajenga kiwanda kikubwa sana cha cement kule kusini (mtwara). Ndio maana unamwona JK alikuwa na mazungumzo naye na sasa ametembelea hiki kiwanda chake.
ReplyDeleteKwa kweli Tanzania tunacheza.A local/domestic investor has really invested!!1 you see the impact to the nation.Hongera Dangote
ReplyDelete