Sehemu ya foleni ya malori ikielekwa kubeba mzigo katika kiwanda  cha Saruji cha Dangote  kilichopo katika eneo la Obajana,  Jimbo la Kogi, kilomita 400 Kaskazini Mashariki mwa mji maarufu wa kibiashara wa Nigeria, Lagos. 
Kwa sasa Kiwanda hicho  kinazalisha tani za kimetriki milioni 10.25 kwa mwaka na hivyo kukifanya kiwanda hicho kuwa kiwanda kikubwa zaidi cha saruji duniani kilichoko katika eneo moja. 
Baada ya upanuzi unaoendelea kufanywa kwenye kiwanda hicho, uwezo wake wa uzalishaji utaongezeka na kufikia tani za kimetriki 13.0 kwa mwaka. Kiwanda hicho kilicho kwenye eneo la kilomita za mraba saba kitakuwa kimegharimu kiasi cha dola za Marekani bilioni 2.5 wakati upanuzi wake utakapokamilika mwakani. Kwa sasa kiwanda hicho kina biashara ya dola za Marekani bilioni mbili kwa mwaka. 
Kiwanda hiki , kilichoanza kujengwa mwaka 2003 na kukamilishwa mwaka 2006,  na hatimaye awamu zake za kwanza na za pili kuzinduliwa rasmi na Rais Olusegun Obasanjo Mei 12, mwaka 2007, wiki mbili kabla ya kustaafu Urais wa Nigeria, kinaajiri watu 800 kwa wakati mmoja na hivyo kuwa miongoni mwa waajiri wakubwa zaidi katika Nigeria.
 Sehemu ya malori yakiwa katika foleni ya kusubiri zamu kuelekea kiwandani kupakia mzigo

 Malori zaidi
Uwanja wa ndege binafsi wa kiwanda cha saruji cha Dangote.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 11, 2014

    Asante kwa "Mapicha ya kumwaga".Vipi Blog ya jamii ilijaribu kupata BEI ya mfuko mmoja wa simenti unagharimu kiasi gani(kwenye dola za kimarekani) nchini Naijeria(Nigeria)??Kwa Tanzania mfuko mmoja wa Simenti unagharimu karibu dola za kimarekani 9.1(kadirio la kiwango cha ubadilishaji fedha=Sh.1645 kwa dola 1 ya Kimarekani) au zaidi,hii ni kwa Daresalaam hadi huko mikoani.Nataka kulinganisha bei tu,nachelea kusema bei ya Simenti Tanzania iko juu sana.Na kila Mtanzania aliyeko nje ya nchi anaweza kutupatia "local price/bag" ya Simenti alipo tulinganishe.Mwisho

    David V

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 11, 2014

    alhajj usipoipata pepo ya Mungu itabidi tu ujilaumu

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 11, 2014

    mi nadhani baba mkwe angemwomba jamaa aje hata >Bagamoyo, manake sehemu za msata kulingana na utafiti kuna malighafi cement nzuri ya kiwango kama cha wazo Hill

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 11, 2014

    Mdau Anonymous hapo juu huyu jamaa tayari yupo bongo anajenga kiwanda kikubwa sana cha cement kule kusini (mtwara). Ndio maana unamwona JK alikuwa na mazungumzo naye na sasa ametembelea hiki kiwanda chake.

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 12, 2014

    Kwa kweli Tanzania tunacheza.A local/domestic investor has really invested!!1 you see the impact to the nation.Hongera Dangote

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...