Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Bw. Amini Mbaga (kulia) akijadiliana
swala na Mwenyekiti wa kituo cha watoto cha Mama wa Huruma, Mtawa Berna Mdendemi
mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam. TTCL ilitoa msaada wa mifuko 70 ya sementi
kuwezesha kituo hicho kuwa na majengo yake.
Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Bw. Amini Mbaga (kushoto)
akiwasalimia watoto wa kituo cha Mama wa Huruma mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
TTCL ilitoa msaada wa mifuko 70 ya sementi kuwezesha kituo hicho kuwa na majengo yake.
Na Mwandishi wetu, Dar es Salaam
Watu binafsi na taasisi mbalimbali nchini zimetakiwa kuendelea kusaidia watoto wanaoishi
katika mazingira magumu ili kuwaendeleza ili hatimaye waje kuwa na mchango kwa taifa.
Wito huo umetolewa na Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Bw. Amini
Mbaga alipokuwa akikabidhi msaada wa saruji wa mifuko 70 kwa ajili ya kukisaidia kituo cha
kituo cha Mama wa Huruma kuwa na majengo yake.
Bw. Mbaga aliwaambia waandishi wa habari jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki kuwa
kampuni yao imetoa saruji hiyo kwa kituo hicho ili watoto waweze kukuzwa katika mazingira
bora na yenye heshima zaidi.
“Pamoja na kutoa huduma ya mawasiliano kwa jamii pia huwa tunashiriki katika maswala ya
kusajidia jamii,”alisema, huku akitoa changamoto kwa wadau wengine kuiga mfano huo.
Kituo hicho kilianzishwa na watawa wa Kanisa Katoliki na kinahudumia watoto hao mahitaji
ya elimu, chakula na malazi ili waweze kuja kuwa raia wema hapo baadaye.
“Watoto hawa wakiachwa wanazagaa mitaani bila ya huduma yoyote ni hatari kwa maisha
yao na taifa...tuwasaidie kwa faida yao na nchi kwa ujumla,” alisema.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kituo hicho Mtawa Berna Mdendemi alisema kituo hicho
kinawatoto 70 ambao hawana wazazi, watoto wa mitaani na wale wanaoishi mazingira
magumu.
“Tuligundua kuwa watoto wengi katika maeneo haya walikuwa wanazagaa na hivyo
tukaguswa na kuamua kuanzisha kituo hiki,”alisema.
Watoto hao wanasaidiwa kupata elimu ya awali, msingi, elimu ya stadi za maisha pamoja na
malazi, chakula, na huduma za afya.
Mipango ya badaye ni kujenga shule ya sekondari na maarifa ya nyumbani ili kusaidia
kuwakomboa watoto hao na kuwa na taifa lenye vijana wanaojiweza.
“Tunaishukuru kampuni ya TTCL kwa msaada wao ambao utatusaidia sana katika ujenzi huu
ambao tumeuanza kwa kiasi fulani,”alisema.
Aliomba watu na taasisi mbalimbali kuendelea kukisaidia kituo hicho ili kiweze kufikia
malengo yake.
Kituo hicho kilicho katika eneo la Madale kilianza mwaka 2010.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...