Baadhi ya wanachama wa Chama Cha mapinduzi (CCM) tawi la chuo cha kimataifa cha Diplomasia wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuanza kwa uchaguzi wa tawi hilo jana jumamosi 24/5/2014.Kutoka kushoto ni Mohamed Mkumbwa,George Fautine,Dk.Telesphory Kyaruzi,Faiza Salim,Kanali Rankho,Mtela Mwampamba,Ali Makwiro na Kennedy Ndosi.Uchaguzi huo ulisimamiwa na Mtela Mwampamba,Kanali Rankho,Dotto Nyirenda,katibu wa CCM mkoa wa vyuo vikuu Bw.Zenda Daniel na katibu wa CCM itikadi na uenezi wa mkoa wa vyuo vikuu Bw. Madebe,pia uliongozwa kwa kanuni zote za chama hicho hadi mwisho ambapo ulimalizika saa tatu na nusu usiku.
Baadhi ya viongozi wa tawi jipya la Chama Cha mapinduzi (CCM) la chuo cha kimataifa cha Diplomasia wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kumalizika kwa uchaguzi wa tawi hilo jana jumamosi 24/5/2014 ambao ulikuwa na ushindani mkubwa wa kisiasa hasa kutokana na chuo hicho kuwa chimbuko la wanadiplomasia wanaoheshimika duniani pamoja na wanasiasa machachari hapa nchini na Duniani kwa ujumla.
Katika uchaguzi huo Dk.Teresphory Kyaruzi alichaguliwa kuwa mwenyekiti wa tawi hilo jipya bila kupingwa,huku Bw.Kennedy Ndosi akichaguliwa kuwa katibu mpya wa tawi baada ya ushindi wa kishindo dhidi ya mpinzani wake Severine Kapinga aliyepata kura 3 dhidi ya 8 za wajumbe wote wa kamati kuu ya tawi. Kutoka kushoto ni Ali Makwiro, Mtela Mwampamba, Dk.Telesphory Kyaruzi, Faiza Salim, Mohamed Mkumbwa,Sixtus Muhaji,Kennedy Ndosi,George Fautine,Bonnah Kalua,Kanali Rankho,George Lupenza na Dotto Nyirenda.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...