Na Anna Nkinda – Maelezo

Wilaya ya Kinondoni kwa kushirikiana na ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam wanaandaa mkakati wa kusafirisha wanafunzi kwa vitambulisho maalum vya wanafunzi kwa bei naafuu kwa kutumia mabasi ya UDA  kwenda shule za pembezoni.

Hayo yamesemwa hivi karibuni na Afisa Elimu Sekondari wilaya ya Kinondoni Omath Sanga wakati akisoma taarifa ya Idara ya Elimu kwa Mke wa Rais Mama Salma Kikwete alipoitembelea shule ya Sekondari ya Kata ya Salma Kikwete iliyopo Kijitonyama wilayani humo.

Sanga alisema wanafunzi hao ambao wanatumia usafiri wa mabasi zaidi ya moja kwenda shule kwa siku kutoka majumbani kwao kuelekea maeneo ya Goba, Fahari, Kinzudi, Mabwe, Kisauke, Njechele, Mabibo, Malambamawili, Hondogo, Gogoni, Kibwegere na Kibweheri mara baada ya kukamilika kwa vitambulisho bivyo watalipa nauli ya shilingi 200 kwenda na 200 kurudi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...