Mheshimiwa Omar Mjenga, Balozi Mdogo wa Tanzania,Dubai leo AMEKUTANA NA MHESHIMIWA GELINA, BALOZI MDOGO WA MALAWI, DUBAI NA UJUMBE WAKE KUTOKA WIZARA YA MAMBO YA NJE YA MALAWI.
Mheshimiwa Omar Mjenga akiwa katika picha ya pamoja na wageni wake. Kulia kwake ni Mheshimiwa Bi Gelina Balozi Mdogo wa Malawi. Na kulia kwa Mheshimiwa Gelina ni Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu (DAP) kutoka wizara ya mambo ya nje ya Malawi. Kushoto kabisa mwa picha ni Mhasibu Mkuu wa wizara hiyo na kulia mwa picha Naibu Mkuu wa Itifaki kutoka wizara ya mambo ya nje ya Malawi.
Mheshimiwa Omar Mjenga akiwa na Bi Gelina Balozi Mdogo wa Malawi Dubai
Mheshimiwa Omar Mjenga na wageni wake, wakiwa katika mazungumzo, ambayo yalilenga kubadilishana mawazo kuhusu uendeshaji wa Balozi Ndogo. Aidha, walizungumzia njia muafaka za kuvutia watalii na uwekezaji katika nchi zao.Ujumbe huu, awali, ulishakutana na Balozi Mdogo wa Afrika Kusini, Angola, Mozambique, Ethiopia, China, India, na Marekani.Wanaendelea na mikutano yao wikiijayo.
Huo kweli ni ubalozi mdogo - literally. Naona viti havitoshi. Watu wamekaa kwa kubanana...
ReplyDeletemdau hapo juu umeumiza mbavu zangu.loh
ReplyDelete