Mheshimiwa Omar Mjenga, Balozi Mdogo wa Tanzania,Dubai leo AMEKUTANA NA MHESHIMIWA GELINA, BALOZI MDOGO WA MALAWI, DUBAI NA UJUMBE WAKE KUTOKA WIZARA YA MAMBO YA NJE YA MALAWI.
Mheshimiwa Omar Mjenga  akiwa katika picha ya pamoja na wageni wake. Kulia kwake ni Mheshimiwa Bi Gelina Balozi Mdogo wa Malawi. Na kulia kwa Mheshimiwa Gelina ni Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu (DAP) kutoka wizara ya mambo ya nje ya Malawi. Kushoto kabisa mwa picha ni Mhasibu Mkuu wa wizara hiyo na kulia mwa picha Naibu Mkuu wa Itifaki kutoka wizara ya mambo ya nje ya Malawi.
Mheshimiwa Omar Mjenga  akiwa na Bi Gelina Balozi Mdogo wa Malawi Dubai
Mheshimiwa Omar Mjenga na wageni wake, wakiwa katika mazungumzo, ambayo yalilenga kubadilishana mawazo kuhusu uendeshaji wa Balozi Ndogo. Aidha, walizungumzia njia muafaka za kuvutia watalii na uwekezaji katika nchi zao.Ujumbe huu, awali, ulishakutana na Balozi Mdogo wa Afrika Kusini, Angola, Mozambique, Ethiopia, China, India, na Marekani.Wanaendelea na mikutano yao wikiijayo.
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 09, 2014

    Huo kweli ni ubalozi mdogo - literally. Naona viti havitoshi. Watu wamekaa kwa kubanana...

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 09, 2014

    mdau hapo juu umeumiza mbavu zangu.loh

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...