Kiongozi wa UKAWA Freeman Mbowe, akihutubia katika mkutano wa hadhara katika viwanja vya Gombani ya Kale, Chake Chake Pemba.
Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi James Mbatia, akihutubia katika mkutano wa hadhara katika viwanja vya Gombani ya Kale, Chake Chake Pemba.
Mwenyekiti wa CUF Prof. Ibrahim Lipumba, akihutubia katika mkutano wa hadhara katika viwanja vya Gombani ya Kale, Chake Chake Pemba.
Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif Sharif Hamad, akihutubia katika mkutano wa hadhara katika viwanja vya Gombani ya Kale, Chake Chake Pemba.
Baadhi ya viongozi wa UKAWA na wananchi wakisikiliza kwa makini hotuba Maalim Seif, katika mkutano wa hadhara uliofanyika viwanja vya Gombani ya Kale, Chake Chake Pemba.
Wafuasi na wapenzi wa vyama vya upinzani wakifuatilia mkutano wa UKAWA uliofanyika viwanja vya Gombani ya Kale, Chake Chake Pemba. (Picha na Salmin Said, OMKR).

BOFYA HAPA KWA HABARI KAMILI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 02, 2014

    Saaafi...tangu juzi nilikua natafuta habari za ukawa hapa globuni...nikaanza kufikiri labda hujaletewa taarifa za maendeleo ya mkutano....kama ambayo huwa mnasemaga.....

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 02, 2014

    Michuzi is so biased, how did this one surfaced here?

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 03, 2014

    UDUGU WA PAKACHA ANKAL...haudumu!!!

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 03, 2014

    UKAWA maana yake nini?

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 03, 2014

    Kumradhi mtoa mada wa kwanza lakini unachokiita saaafi ni nini?
    Ujinga haupigiwi debe ndugu yangu. Na huu wa ukawa ni zaidi ya ujinga. Tunakokusudia kwenda ni mbali sana lakini hawa ukawa wanapambana kuhakikisha safari yetu watanzania haifanikiwi.
    Hawa ni maadui na sumu mbaya sana. Ni wahaini wanaotumia mbinu zote kuwadhuru wananchi kwa ajili tu ya kufanikisha maslahi yao ya kisiasa. Umoja usio na kibali umepata wapi pesa za kuzunguka nchi nzima kuvuruga uundwaji wa katiba?
    Lazima Serikali ipige marufuku kampeni zozote zenye lengo la kuharibu juhudi za kutunga katiba mpya. Pia namwomba Rais awavue viongozi wote wa ukawa ubunge wa bunge la katiba ili wengine wachukue nafasi zao bungeni na wao waendelee na kampeni laana za kuvuruga vichwa mitaani.
    Mndengereko Ukerewe

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 03, 2014

    Ni hatari sana kuyaita mawazo ya mabadiliko na mapinduzi UJINGA.Siku zote watu wasiotaka mabadiliko (CONSERVATIVES)ukiwachunguza kwa makini ni wale wanolinda masilahi yao katika mfumo dhalimu uliopo.
    Jamani wana CCM mnatakiwa kuwa wepesi wa kusoma mabadiliko ya majira na nyakati (wind of changes) ili mtafute cha kufanya kitakochoendana na wakati
    kuliko kuendelea na mawazo yenu mgando, kutukana, kukashifu, kukejeli na kusambaza propaganda kama huyo jamaa hapo juu.

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 03, 2014

    Duh! Mabadiliko ya kimapinduzi!
    Kwani kukimbia bunge ni mabadiliko ya kimapinduzi?
    Isije tukawa tunashabikia issue kwa kuangalia sura?
    Maana mimi sioni kama wanachokifanya waliokimbia kikao halali bungeni ni kuleta mabadiliko ya kimapinduzi.
    Na sielewi ni vipi mpinzani wa uamuzi wa kutoroka bungeni aonekane ni mwana ccm.
    Kwani Lipumba na Lissu na Mbowe hawapingwi ila na wana ccm tu?
    Tuna tatizo la uchache na uvivu wa kufikiri Tanzania, na si kwa kila mtanzania bali kwa wachache wanaodhani kuwa unapotofautiana na wanasiasa wanaowaabudu wao basi wewe ni ccm na hoja zako ni kashfa, kejeli, matusi au propaganda.
    Hao ni watumwa wa kujitakia, wajihakiki.
    Mdau Ughaibuni

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...