Kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania imeshinda tuzo ya nafasi ya kwanza ya Usalama na Afya Mahala pa kazi kwa mwaka 2014 kwa upande wa sekta ya mawasilinao ikiwa ni mara ya kwanza kwa kampuni hiyo kushinda tuzo hiyo tangu ilipoanzishwa mwaka 2000.

Tuzo hiyo inayotolewa na Mamlaka ya Usalama na Afya Mahala pa kazi Nchini (OSHA) imetolewa wakati wa maadhimisho ya kilele cha siku ya Usalama na Afya Mahala pa kazi Duniani ambapo kitaifa ilifanyika jijini Dar es salaam wiki iliyopita.

Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Rene Meza amesema ushindi wa tuzo hiyo iliyokabidhiwa kwa Vodacom na Makamu Wa Rais Dk. Mohamed Gharib Bilal ni matokeo ya juhudi za makusudi ambazo Vodacom imekuwa ikiziweka katika kulinda,kuhamasiha na kuimarisha usalama na faya za wafanyakazi wake.

Amesema kwa Vodacom sula la usalama na afya ya mfanyakazi ni jambo lisilokuwa na mbadala na kwamba mkazo mkubwa unawekwa katika eneo hilo kwa wafanyakazi pamoja na wakandarasi na watoa huduma wengine wa Vodacom.

“Tunawashukuru sana wafanyakazi wetu na pia wadau wetu kwa kuunga mkono sera, mikakati na miongozo yetu inayolenga kuhimizana na kukumbushana miongoni mwetu umuhimu wa kuzingatia bila shuruti usalama na afya ya kila mmoja wetu wakati tunapotimiza majumuku yetu, bila yao tuzo hii isingekuwa rahisi kwetu kuipata.”Alisema Meza

“Unaweza kuona jinsi watu walivyo salama katikakati ya shughuli zetu zinazohusisha kandarasi za ujenzi wa minara, wafanyakazi wetu wetu wanatumia vyombo vya usafiri katika kutekeleza majukumu yao n.k hivyo ni jambo lenye kufurahisha kuona kwamba yote hayo yanafanyika pasi na kuhatarisha usalama na afya zao ni kutufikisha kushinda tuzo “Aliongea Meza

Amesema kwa kushinda tuzo hiyo, OSHA imetambua mchango wa Vodacom katika kutoa mchango wake wa kuhakikisha kunakuwepo na utekelezaji wa miongozo yenye kulinda usalama na afya ya mfanyakazi wakati wote anapotimiza majukumu yake kwa mwajiri.

Meza amesema kampuni ya Vodacom inatoa kipaumbele na mkazo mkubwa katika eneo la usalama na afya mahala pa kazi kwa wafanyakazi ikiamini kuwa kwa kufanya hivyo kunachangia pia kuongeza ufanisi kwa wafanyakazi huku wakijilinda na kwa faida zao na familia zao.

“Kila wakati tunawaeleza na kuwakumbusha wafanyakazi wetu kwamba usalama na afya zao kwanza kwa kuwa kampuni inawahitaji na familia zao zinawategemea, kampuni inafanya kila lililo ndani ya uwezo wake na wao kwa upande wao wanapokea na kutii yale tunayokumbushana. Hii ndio siri ya ushindi wetu.”Amesema

Hii ni tuzo ya nne ya kitaifa kwa kampuni ya Vodacom katika kipindi cha nusu mwaka. Tuzo nyengine ambazo Vodacom imeshinda hivi karibuni ni Tuzo ya mwajiri bora wa mwaka iliyotolewa na TEA, Tuzo ya mlipa kodi mkubwa wa mwaka katika sekta ya mawasiliano kutoka TRA pamoja na tuzo ya mlipa kodi mkuu wa tatu kitaifa pia kutoka TRA,

Kuhusu mipango katika miezi michache ijayo, Meza amesema mbali na kutimiza wajibu wake kwa wadau wote wa ndani na nje wakiwemo wateja na wafanyakazi, Vodacom itaendelea kuwa mwezeshaji mkuu wa huduma za mawasiliano ya simu za mkononi  nchini kupitia teknolojia bora.

Kwa sasa Vodacom inawafikia watanzania zaidi ya 90% huku ikiongeza mtandao wake wa teknolojia ya 3G kuwezesha watanzania wengi zaidi kuwa na huduma za Intaneti na pia kuwezesha huduma mtandao katika biashara, elimu, kilimo, afya na huduma nyengine mbalimbali za kiuchumi na kijamii.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...