Na Nathan Mtega wa demashonews,Songea
SERIKALI ya mkoa wa Ruvuma imeendelea kuwasihi wafanyakazi wa sekta zote nchini wasijenge zaidi utamaduni wa kudai haki bila kutimiza wajibuwao kwanza kwa sababu kauli mbiu za vyama vingi vya wqafanyakazi kikiwemo chama cha walimu nchini ambacho kauli mbiu yake  ni wajibu na haki.
 Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo,Mh. Abdula Lutavi
 -----------------
Kauili hiyo imetolewa na mkuu wa wilaya ya Namtumbo Abdula Lutavi kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Ruvuma kwenye maadhimisho ya siku ya wafanyakazi yaliyofanyika kimkoa katika uwanja wa Maji maji mjini Songea ambapo amesema baadhi ya wafanyakazi wakiwemo walimu wamekuwa hawatimizi wajibu wao ipasavyo lakini ndiyo wanakuwa msitari wa mbele kulaumu na kudai haki pasipo kutimiza wajibu wao kwanza kwa mwajiri.
Wanafunzi wa Chuo cha VETA Songea wakipita mbele ya jukwaa kuu huku wakionyesha mavazi wanayoshona chuoni hapo ikiwemo mavazi la maharusi na ya ulimbwende.
-----------------------------------
Amesema sekta ya elimu ndiyo yenye watumishi wengi ambao wapo katika kila kijiji nchini na ndiyo wataalamu wanaotumiwa na wananchi wa maeneo hayo lakini baadhi yao wamekuwa ni watoro na wazembe katika maeneo yao ya kazi na kutotimiza wajibu wao kwa makusudi na kwa visingizio mbali mbali na wakiendelea kulindwa na walimu wakuu pamoja na wakuu wa idara za kielimu hali ambayo inazidi kudumaza kiwango cha elimu mkoani Ruvuma na kuufanya mkoa kuendelea kutofanya vizuri katika sekta hiyo muhimu.

BOFYA HAPA KWA PICHA NA HABARI KAMILI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 02, 2014

    Mafundi wa ushonaji Ruvuma wanajitahidi..

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...