Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd (kulia) akipokea msaada wa sh milioni mbili kutoka kwa Meneja wa NBC tawi la Zanzibar, Rajab Maalim (kushoto) zilizochangwa na wafanyakazi wa benki hiyo kwa ajili ya timu ya watoto wenye ulemavu wa akili watakaoshiriki michezo ya olimpiki maalumu inayotarajiwa kuanza Juni 6 mwaka huu Wilayani Kibaha katika Mkoa wa Pwani. makabidhiano yalifanyika kwenye ofisi za makamu wa rais, Vuga, Zanzibar jana
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, : Balozi Seif Ali Idd akikabidhi fedha zilizochangwa na wafanyakazi wa NBC nchini pamoja na yeye mwenyewe kwa Makamu Mwenyekiti wa Kamati Maalumu ya Olimpiki Zanzibar, Saada Hamad katika hafla hiyo mjini Zanzibar.
Baadhi ya watoto wenye ulemavu wa akili watakaoshiriki michuano hiyo wakiwa katika hafla hiyo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...