Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiki akiungana na Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda walipoungana na wananchi kufanya usafi katika mto wa Mlalakuwa jijini Dar es Salaam ili kuepukana na ugonjwa uliozuka wa Dengue ambao umekuwa tishio wakati akizindua zoezi la kufanya usafi jijini lililokwenda kwa jina la ‘MLALAKUWA MTO WETU, AFYA YETU’ lililofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita.
 Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda (kushoto) akimuongoza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiki (katikati) kukagua  mto wa Mlalakuwa jijini Dar es Salaam wakati akizindua zoezi la kufanya usafi lililokwenda kwa jina la ‘MLALAKUWA MTO WETU, AFYA YETU’ lililofanyika lililofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita.
 Wakati zoezi la kukagua mto wa Mlalakuwa, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiki na Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda walipata wasaa wa kupita na kumpa pole mkazi wa Mikocheni ambaye alikuwa amefiwa na Shemeji yake.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiki (mbele) akiongozana na Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda kuvuka Mto Mlalakuwa kuongea na wananchi waliokuwa ng'ambo ya mto.

BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 20, 2014

    Hongereni, nendeni na pale shoko (Lugalo) mkazuie uchimbaji wa mchanga au mpaka daraja liondoke?

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 20, 2014

    wewe mdau acha unoko, usisikie hakuna wa kutugusa hapa wenyewe wanatujua.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 20, 2014

    Na haya mafuriko ya kiangazi! lazima hilo daraja liondoke tu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...