Meneja Uendeshaji wa pitiaAirtel Money Asupya Naligingwa (kushoto) akiongea wakati wa uzinduzii wa ushirikiano kati ya Airtel na Precision Air utakaowawezesha wateja wa Airtel kulipia tiketi za ndege kupitita huduma ya Airtel Money. akishuhudia ni Afisa uhusiano wa Airtel bi Jane Matinde na na Afisa masoko wa Precision Air Hillary Mremi
Meneja Uendeshaji wa pitiaAirtel Money Asupya Naligingwa (kushoto) na Afisa masoko wa Precision Air Hillary Mremi (kulia) kwa pamoja wakizindua ushirikiano kati ya Airtel na Precision Air utakaowawezesha wateja wa Airtel kulipia tiketi za ndege kupitita huduma ya Airtel Money. akishuhudia ni Afisa uhusiano wa Airtel bi Jane Matinde.
kampuni ya simu za mkononi ya Airtel imeanzisha ushirikiano na Precision Airtel utakaowawezesha wateja wake nchi nzima kununua tiketi za ndege kupitia huduma ya Airtel Money
Ushirikiano huu utawapatia wateja wa Precision Air urahisi katika kupanga safari zao na kuwawezesha kununua ticket zao wakati wowote bila usumbufu kupitia huduma ya Airtel Money.
Akionge wakati wa uzinduzi Afisa Uhusiano wa Airtel Bi Jane Matinde alisema “ushirikiano huu utawapatia wateja wetu wa Airtel njia mbadala, rahisi naya uhakika ya kulipia safari zao za ndani na za nje huku ikiwapatia watanzania na wateja wetu uzoefu tofauti wa kufanya malipo ya tiketi zao za ndege kupitia simu zao za kiganjani. Kwa kupitia huduma hii mpya sasa wateja wetu wataweza kufanya malipo ya tiketi zao za ndege mahali popote kwa usalama na haraka zaidi kupitia huduma ya Airtel Money. ”
“Tutaendelea kuthibitisha dhamira yetu ya kutoa bidhaa na huduma za kibunifu huku tukiwahakikishia wateja wetu huduma bora kupitia huduma ya Airtel Money na nyinginezo wakati wote”. Aliongeza Matinde
Akiongelea kuhusu ushirikiano huo Afisa Masoko wa Precision Air Bwana Hillary Mremi alisema “ ushirikiano huu umekuwa kwa wakati muafaka wakati Precision Air imejipanga kuboresha huduma zetu na kuwapatia wateja wetu uzoefu tofauti katika huduma za ndege huku tukihakikisha wateja wanafurahia huduma zetu zinazoenda zaidi ya matarajio yao.
Wateja wetu sasa wanaweza kufanya malipo ya tiketi zao za ndege kwa kupitia huduma ya Airtel Money . kupitia simu zao za mkononi wateja wetu wanaweza kupiga call center au kutembelea tovuti yetu kufanya booking ya safari zao na kulipia kupitia Airtel Money na kisha kupokea tiketi yako kupitia simu yako ya mkononi” aliongeza Mremi.
Akiongea kuhusu namna ya kupata huduma hiyo Meneja uendeshaji wa Airtel Money Asupya Naligingwa alisema” huduma hii ni rahisi kutumia , mteja anachotakiwa kufanya ni kupiga simu na kufanya booking ya safari au kufanya booking kupitia tovuti ya Precision Air ambapo mteja atapewa namba ambayo itatumika kama reference wakati wa malipo.
Kununua tiketi kupitia Airtel Money wateja wanatakiwa kufanya yafuatayo
Piga *150*60#
Chagua namba 5 (Lipia Bili)
Chagua namba 8 (NYINGINEZO)
Andika jina la biashara
PW
Ingiza Kiasi cha pesa
Kumbukumbu rejea
(namba ya booking)
Ingiza neno la siri kulipa PW, Tsh xxxxx, kumbukumbu rejea namba xxxxxx
Baada ya kufanya hayo utapokea ujumbe wenye uthibitisho wa malipo na tiketi yake ya ndege “aliongeza Nalingingwa.
Huduma ya Airtel Money ni huduma inayowawezesha wateja wa Airtel Nchi nzima kufanya malipo na miamala ya pesa kupitia pesa simu ya mkononi . kwa kupitia huduma ya Airtel money wateja wanaweza kulipia ankra kama vile DAWASCO, LUKU, USA visa, DSTV, kulipia mikopo , kununua muda wa maongezi, kununua vifurushi vya yatosha na kutuma na kupokea pesa kutoka kwa marafiki na familia na huduma nyingine nyingi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...