Na Sylvester Onesmo 
wa Jeshi la Polisi, Dodoma.

Watu wawili wamepoteza maisha kutokana na ajali mbili zilizotokea katika maeneo mawili tofauti na nyakati tofauti Mkoani Dodoma.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi DAVID MISIME – SACP (pichani) ameeleza kuwa, ajali ya kwanza ilitokea tarehe 30/05/2014 majira ya saa 18:30hrs katika kijiji cha Ipala Wilaya ya Dodoma ambapo gari lenye namba za usajili DFP 614 Toyota Land Cruiser mali ya chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo likitokea chuoni kuelekea Dodoma mjini likiendeshwa na ALFRED S/O MLIGO, MIAKA 35, MHEHE, liliacha njia na kupinduka na kusababisha kifo chake.  Pia watu watano walipata maumivu mbalimbali na walitibiwa na kuruhusiwa. 

Mwili wa marehemu upo katika Hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Dodoma kusubiri taratibu nyingine.

Kamanda MISIME AMESEMA ajali ya pili imetokea majira ya saa 18:45hrs huko katika kijiji cha SILWA barabara ya Dodoma – Morogoro ambapo gari lenye namba za usajili T.150 CWA Toyota Granvia Station Wagon likiendeshwa na MGENI S/O SHEMAKAME, MBONDEI, MIAKA 29 MKAZI WA MBURAHATI DSM liliacha njia na kusababisha kifo cha GEORGE S/O TYSON, MIAKA 39, MWANAHABARI, Mkazi wa mbezi DSM.

Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Wilaya ya Gairo ukisubiri taratibu za Polisi na wanandugu. 

Pia katika ajali hiyo wanahabari wanne (4) wa Mboni show walipata majeraha mbalimbali na kutibiwa na kuruhusiwa, ambao ni:-

1.   NIXON S/O KABUMBILE, MHAYA, MIAKA 31
2.   GRACE D/O MEENA, MCHAGA, MIAKA 28
3.   NTWA S/O KABOLE, MNYAKYUSA, MIAKA 33
4.   JUSTINE S/O BAYO, MIAKA 27, MMASAI
 Uchunguzi wa awali unaonyesha ajali zote mbili zimesababishwa na mwendokasi. Kamanda MISIME ametoa wito kwa madereva kuepuka mwendokasi na kuwa na udereva wa kujihami ambao unasaidia dereva kusimama bila kusababisha madhara linapotokea jambo lolote na hata kama ajali ikitokea madhara hayawezi kuwa makubwa kama yanavyokuwa anapokuwa kwenye mwendo wa kasi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 31, 2014

    Duuh hii Kali tangu lini watanzania wanaitana na makabila yao ???...RIP Ndugu zetu na poleni sana wafiwa na najeruhi pia Mungu awape nguvu katika kipindi hiki kigumu..tukumbukeni tusimsahau Mungu katika maisha yetu ya kila siku.
    AMEN!!

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 31, 2014

    Miaka yote tunatambulika kwa majina, miaka na sehemu unayoishi. Hivi sasa kila nikisoma taarifa ya polisi lazima utaona na kabila la muhusika. Hii si dalili nzuri. Taratibu ukabila utashamiri katika nyanja mbalimnbali na tutaelekea pabaya ndugu zangu ikiwa vyombo vya dola vimeanza kushika kidedea suala hili. Ukabila ni mwiko Tanzania. Tunatambulika kwa majina yetu ya ukoo kwisha.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 01, 2014

    Natoa pole kwa waliofiwa na majeruhi pia.

    Hili la kuamdika makabila kama lina tija kwa maafisa polisi basi liishie hukohuko kwao.Sisi wananchi majina na umri vinatutosha.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 01, 2014

    RIP GEORGE.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...