Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (kulia) akipokea pongezi kutoka kwa
Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Mbarak Abdulwakil (kushoto) na Naibu Katibu Mkuu,
Mwamini Malemi (katikati) mara baada ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania kuipitisha Bajeti ya Wizara hiyo katika Bunge la Bajeti linaloendelea
mjini Dodoma. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Mkurugenzi
wa Idara ya Sera na Mipango, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Haji Janabi
(kushoto) akimpongeza Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame
Silima (kulia) kwa kuyajibu kwa ufasaha baadhi ya maswali ya Waheshimiwa Wabunge
na hatimaye Bajeti ya wizara hiyo ya Mwaka wa Fedha 2014/15 kupita. Kulia kwa
Naibu Waziri Silima ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Mbarak Abdulwakil na Naibu
Katibu Mkuu, Mwamini Malemi.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (wapili kulia) akimfafanulia Mkuu wa
Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu, jinsi alivyoyajibu maswali ya
waheshimiwa wabunge kabla ya kupitishwa Bajeti ya wizara hiyo ya Mwaka wa Fedha
2014/15.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (kulia) wakipongezana na Naibu
Waziri wa Wizara hiyo, Pereira Ame Silima kwa kuyajibu maswali mbalimbali ya
waheshimiwa wabunge na hatimaye Bajeti ya wizara yao kupitishwa na Bunge la
Bajeti linaloendelea mjini Dodoma. Nyuma yao, Kulia ni Katibu Mkuu wa wizara
hiyo, Mbarak Abdulwakil na Naibu Katibu Mkuu, Mwamini Malemi. Picha na Felix
Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...