Wachezaji wa Atlético Madrid wakishangilia ushindi wao dhidi ya Barcelona jana. Baada ya kuisambaratisha Real Madrid katika uwanja wao wa Santiago Bernabeu na kunyakua kombe la Copa del Rey (Kombe la Mfalme) mwaka uliopita, Atlético Madrid jana wamefanya maajabu mengine baada ya kunyakua ubingwa wa La Liga mkononi mwa Barcelona ya kina Messi kwa kutoka nao droo ya 1-1.
Ni ubingwa wao wa kwanza katika miaka 18. Kifuatacho ni kucheza fainali za mabingwa wa Ulaya baada ya miaka 40! Mambo hayo ya Diego Simeone na timu yake hiyo si ya kawaida. Hata mashabiki wa Barca walilitambua hilo baada ya filimbi ya mwisho ambapo waliinuka na kuwashangilia.
Huyo anaitwa Diego Simeone aka Cholo...Bado na ubingwa!
ReplyDeleteSasa sijui waspain kwanini wanamuita cholo?! Sijui cholo huyu huyu wa kwetu Zenji?!