Mwandishi
wa Habari kutoka Gazeti la ‘The West Australian’ Kim MacDonald, akiandika
maelezo yaliyokuwa yakitolewa na Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter
Muhongo alipofanya mahojiano naye mapema leo ofisini kwake jijini Dar es
Salaam.
“Serikali
ya Tanzania imejipanga vipi katika kuhakikisha gesi asili inayoendelea
kugunduliwa nchini inakuwa yenye manufaa kwa nchi?” Ndivyo anavyouliza
Mwandishi huyo
“Moja
ya mikakati yetu ni kuhakikisha asilimia 75 ya Watanzania wanapata umeme wa
uhakika ifikapo mwaka 2025 ili kuondokana na umaskini”. Ndivyo Waziri wa
Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo anavyomweleza Mwandishi wa gazeti la
“The West Australian’ Kim MacDonald, wakati alipohojiwa na Mwandishi huyo
mapema leo ofisini kwake jijini Dar es Salaam.
huo uvaaji wa huyo mama si unaweza kuleta shida hata waziri wetu akachanganya mada?
ReplyDeleteWewe anon wa hapo juu.Uvaaji huu hauna matatizo, waziri atapata shida gani? Lini mtaacha mawazo ya ngono na mkaendelea kufanya kazi ya kujiletea maendeleo, wewe anon ukitumia asilimia 100 ya mawazo yako kwenye ngono hutajiletea maendeleo na unaweza ukajikuta ukifungwa maisha kwa kubaka. Acha hayo mawazo ya kila wakati na kila mahali yanayohusu ngono, Hayo mawazo yako ungeyapeleka kwenye maendeleo ungefika mbali.
ReplyDeleteLOL!
ReplyDeleteJamani mimi nilikuwa naenda ofisi moja ya serikali nilivaa gauni kama hiyo wakanikatalia kuingia eti kuna "dress code". Sasa huyu mama ameingiaje ofisini kwa waziri kama hivi?
ReplyDeletenaunga mkono mdau namba 1.
ReplyDelete