Mwandishi wa Habari kutoka Gazeti la ‘The West Australian’ Kim MacDonald, akiandika maelezo yaliyokuwa yakitolewa na Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo alipofanya mahojiano naye mapema leo ofisini kwake jijini Dar es Salaam.

“Serikali ya Tanzania imejipanga vipi katika kuhakikisha gesi asili inayoendelea kugunduliwa nchini inakuwa yenye manufaa kwa nchi?” Ndivyo anavyouliza Mwandishi huyo
“Moja ya mikakati yetu ni kuhakikisha asilimia 75 ya Watanzania wanapata umeme wa uhakika ifikapo mwaka 2025 ili kuondokana na umaskini”. Ndivyo Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo anavyomweleza Mwandishi wa gazeti la “The West Australian’ Kim MacDonald, wakati alipohojiwa na Mwandishi huyo mapema leo ofisini kwake jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 12, 2014

    huo uvaaji wa huyo mama si unaweza kuleta shida hata waziri wetu akachanganya mada?

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 12, 2014

    Wewe anon wa hapo juu.Uvaaji huu hauna matatizo, waziri atapata shida gani? Lini mtaacha mawazo ya ngono na mkaendelea kufanya kazi ya kujiletea maendeleo, wewe anon ukitumia asilimia 100 ya mawazo yako kwenye ngono hutajiletea maendeleo na unaweza ukajikuta ukifungwa maisha kwa kubaka. Acha hayo mawazo ya kila wakati na kila mahali yanayohusu ngono, Hayo mawazo yako ungeyapeleka kwenye maendeleo ungefika mbali.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 13, 2014

    Jamani mimi nilikuwa naenda ofisi moja ya serikali nilivaa gauni kama hiyo wakanikatalia kuingia eti kuna "dress code". Sasa huyu mama ameingiaje ofisini kwa waziri kama hivi?

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 14, 2014

    naunga mkono mdau namba 1.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...