Je muziki wako ni wa laivu?
Je muziki wako umehusiana na Africa, Uarabuni au nchi za bahari hindi?
Je umevutiwa kupiga muziki mwezi ujao wa Februari Zanzibar?
Kama unaweza kujibu ndio, ndio, ndio - basi endelea kusoma...
MWISHO wa kupokea maombi - 31 Julai 2014
Kwa wasanii watakao shiriki katika tamasha, kwa kawaida hulipwa pesa kwa ajiri ya onyesho na matumizi yao wakiwa Zanzibar, ikiwa ni usafiri, malazi,chakula na matumizi madogo madogo. Kwa wasanii kutoka nje kawaida wanatakiwa kutafuta wadhamini wao wenyewe kwa ajili ya usafiri
Jopo la uchaguzi litakutana mwanzoni mwa mwezi wa nane kuchagua wasanii watakao shiriki katika tamasha la Sauti za Busara 2015. Wasanii wotewatajulishwa maamuzi ya jopo kwa kupitia barua pepe mnamo mwezi tisa.
Jinsi ya kuomba kushiriki katika tamasha la Sauti za Busara 2015
Maombi yako yatashughulikiwa endapo tutapokea maombi yaliyokamilika kutoka kwako kabla ya tarehe ya MWISHO ya kutuma maombi. Maombi yakolazima yaambatanishwe na vitu vifuatavyo:
form ya maombi iliyojazwa na maelezo mafupi (maneno yasizidi 1000)
nakala moja au mbili ya kazi zako (CD au DVD)
picha moja au mbili(Picha zinaweza kutumwa kwa journey@busara.or.tz)
Tafadhali tuma nakala, picha na maelezo kupitia anwani yetu ya ofisini kama inavyoonekana hapo chini. Vitu vyote vitakavyotumwa lazima viaandikweFOR PROMOTIONAL USE ONLY. Bonyeza hapa kwa fomu ya maombi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...