Pamoja na kupigwa marufuku mara kadhaa wachimabji hawa bado wameendelea kuchimba mchanga katika Mto Mbezi huku wakijaza magari makubwa yasiyo na idadi na tena wakifanya kazi hii mchana kweupeeee pyeeee bila hata kuwa na woga.
Wachimbaji hawa wamekuwa wakifanya hivi kila inaponyesha mvua kubwa inayokusanya mchanga mwingi kutoka eneo jingine kusogeza eneo hili, na wao wamekuwa wakiuhamisha mchanga huo kwa kuuchimba na kuupakia katika magari na kisha kwenda kuuza. Zoezi hili linachangia mmomonyoko mkubwa wa kingo za mto huo ambako nyumba kibao zipo.
Wachimbaji wakiendelea na kazi...
Si kama hawaonekani, si kama ni ngumu kuwazuia, isipokua wenye mamlaka hawana njia mbadala ya kuwafanya watoke na wasirudi tena kuifanya kazi hiyo......
ReplyDeleteSasa wakale wapi? Bora wapige kazi kuliko waingie mtaani na kuanza kukaba na kuiba.
ReplyDeleteNDIO VIZURI SANA TENA SANA,MFEREJI UNAPOKUWA NA MCHANGA AU MTO WA MAJI,UNATAKIWA UTOLEWE MCHANGA MAJI YASIENDE PEMBENI
ReplyDeletebora hawa kuliko viongozi wala rushwa
ReplyDelete