Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania Sunil Colaso akiongea wakati wa uzinduzi rasmi ya Airtel Rising Stars 2014 jijini Dar es Salaam jana.

Mkuuu wa Idara ya Mawasiliano wa Airtel Tanzania Beatrice Singano Mallya akiongea wakati wa uzinduzi rasmi ya Airtel Rising Stars 2014 jijini Dar es Salaam jana.
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) Jamal Malinzi akiongea wakati wa uzinduzi wa Airtel Rising Stars 2014 jijini Dar es Salaam jana. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania Sunil Colaso.

 Dar es Salaam, Jumatatu Juni 23, 2014…Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania leo imezindua rasmi msimu wa nne wa mashindano ya soka kwa vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel Rising Stars ambayo yataanza kutimua vumbi Julai 7 katika ngazi ya awali na kuhitimishwa kwa fainali za Kitaifa jijini Dar es Salaam kuanzia Agosti 3 hadi 10 mwaka huu.

Akiongea na waandishi wa habari kwenye hafla ya uzinduzi jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania Sunil Colaso amesema kampuni ya Airtel Tanzania  ina nia thabiti ya kusaidia maendeleo ya mchezo wa mpira wa miguu hapa nchini na kujivunia mafanikio yaliyotokana na michuano hiyo kwa miaka mitatu iliyopita.

 “Tunaona fahari kwamba michuano ya Airtel Rising Stars imeweza kuibua vipaji vya wachezaji ambao baadhi yao wamechaguliwa kujiunga na timu za taifa za vijana chini ya umri wa miaka 20”, alisema Colaso. Kumbu kumbu za TFF zinaonyesha kwamba timu ya taifa ya wanawake imeundwa na wachezaji wengi kutoka Airtel Rising Stars ambayo madhumuni yake makubwa ni kuibua na kuendeleza vipaji vya soka kwa vijana wenye umri chini ya miaka 17.

Huu ni mwaka wa nne mfululizo kwa michuano ya Airtel Rising Stars kufanyika hapa nchini Tanzania ambayo huanzia ngazi ya chini hadi Taifa. Mashindano ya taifa hutoa wachezaji nyota ambao huenda kupeperusha bendera ya Taifa kwenye michuano ya kimataifa ambayo hujumuisha wachezaji nyota kutoka pande zote za Afrika ambako ARS hufanyika.

Mwaka jana, michuano ya Airtel Rising Stars ya kimataifa ilifanyika nchini Nigeria ambapo Niger iliibuka bingwa kwa upande wa wavulana na Tanzania kutwaa taji la ubingwa kwa timu za wasichana. Mwaka huu michuano ya ARS itajumuisha mikoa ya Mwanza, Morogoro, Mbeya, Temeke, Ilala na Kinonondoni kwa upande wa wavulana na wasichana watawakilishwa na mikoa ya Mwanza, Zanzibar, Mbeya, Temeke, Ilala na Kinondoni.

Colaso pia aliipongeza Shirikisho la Mpira wa miguu Tanzania (TFF) pamoja na serikali kupitia Wizara ya Michezo kwa kuungana mkono  kwa dhati michuano ya Airtel Rising Stars tangu ilipoanzishwa nchini mwaka 2011.

Kwa upande wake, Rais wa TFF Jamal Malinzi aliipongeza Airtel Tanzania kwa kuwekeza kwenye soka la vijana. “Nawapongeza sana kampuni ya Airtel Tanzania kwa mpango wake huu wa kuwekeza kwenye soka la vijana ambayo kwa kweli ndio msingi wa maendeleo wa mpira wa miguu hapa Tanzania na duniani kote”, alisema.

Airtel ni kampuni ya simu za mkononi yenye matawi barani Afrika katika nchi za Burkina Fasso, Chad, Congo, Brazzaville, DRC, Gabon, Ghana, Kenye, Madagascar, Malawi, Niger, Nigeria, Rwanda, Selisheli, Sierra-Leone, Tanzania, Uganda na Zambia.  

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...