Na John Gagarini, Bagamoyo.

MSICHANA Selitian Nata (25) mkazi wa Kijiji cha Kisogo kata ya Vigwaza Wilayani Bagamoyo mkoani Pwani yuko kwenye hali mbaya ya kiafya baada ya kuvimba mguu na kuwa kwenye maumivu makali.Ugonjwa huo uvimbe huo ulianza kama kipele kidogo miaka zaidi ya 10  iliyopita lakini kadiri siku zilivyokuwa zikienda ndipo uvimbe huo ulizidi kuongezeka na kufikia usawa wa mbavu.

Akizungumza na waandishiw ahabari ambao walimtembelea nyumbani kwao alisema kuwa uvimbe huo una ambatana na maumivu makali pamoja na homa kali hasa nyakati za usiku.

“Niko kwenye wakati mgumu kama mnavyoniona napata shida naomba nisaidiwe kwani nimekwenda hospitali toka kipindi hicho lakini sikupata matibabu zaidi ya kupewa vidonge tu ambavyo hupunguza maumivu lakini uvimbe uko pale pale,” alisema Nata.

Nata ambaye ana mtoto mmoja wa kike mwenye umri wa miaka (2) alisema kuwa wakati tatizo hilo linaanza alikwenda hospitali mbalimbali lakini hakuweza kupatiwa matibabu sahihi na kupelekea uvimbe huo kuongezeka hadi hapo ulipofikia na kumkosesha raha.

“Naomba wataalamu mbalimbali pamoja na wafadhili ili niweze kupata matibabu sahihi ambayo yataondoa uvimbe huu ili name niweze kuishi kwa raha kama wengine,” alisema Nata.

Kwa upande wa baba yake Nata Mumbi alisema kuwa alimpeleka mwanae kwenye hospitali mbalimbali kwa ajili ya matibabu lakini hakuna mafanikio yoyote.“Tatizo matibabu ambayo wanayompa si ya kina jambo ambalo linasababisha mwanangu asipate nafuu, lakini kupitia vyombo vya habari naomba wasamaria wema wamsaidie mwanangu ili aweze kupata matibabu sahihi,” alisema Mumbi.

Aidha alisema kuwa anashangaa kuona kila anapokwenda hospitali mwanae anapewa vidonge tu jambo ambalo linafanya wakate tamaa ya kumpatia matibabu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 24, 2014

    The mdudu,madactari wa tanzania ni washenzi sn nawachukia sn because nashindwa kuwaelewa why? Huyu binti anakuakatika hari hii? Kama angekua haendi hospitalini sawa tungesema makosa ni yake lakini yeye mwenyewe pamoja na mzazi wake wanasema wakienda hopitalini wanapewa vidonge tu pasipo na uchunguzi wa kina SASA TUJIULIZENI NINI MAANA YA DACTARI? Hii ni aibu kubwa kwenu tunaomba mbadilike na utendaji wenu wa kishenzi.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 25, 2014

    HOW DO WE DONATE NAJUA KIDOGO KIDOGO HUJAZA KIBABA.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...