Katibu
Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue ambaye pia ni mgeni rasmi akifungua
mkutano mkuu wa mwaka wa Wakurugenzi wa Utawala na Rasilimaliwatu
Serikalini katika ukumbi wa St. Gasper mjini Dodoma leo.
Kaimu Mkuu Mkoa wa Dodoma Bi Fatma Salum Ally (katikati) akiwakaribisha wageni waalikwa wa mkutanomkuu wa mwaka wa Wakurugenzi wa Utawala na Rasilimaliwatu Serikalini mkoani Dodoma, kabla ya mgeni rasmi Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue (kulia) kufungua mkutano huo katika ukumbi wa St. Gasper mjini Dodoma leo.Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-Utumishi Bw. HAB Mkwizu .
Katibu Mkuu Ofisi Rais, Utumishi wa Umma Bw.George D. Yambesi (katikati) akimkaribisha mgeni rasmi Balozi Ombeni Sefue (kushoto) kufungua mkutano mkuu wa mwaka wa Wakurugenzi wa Utawala na Rasilimaliwatu Serikalini katika ukumbi wa St. Gasper mjini Dodoma leo.Kulia ni Katibu wa Tume ya Utumishi wa Umma Bi.Claudia Mpangala.
Baadhi ya washiriki wa mkutano wa mkuu wa mwaka wa Wakurugenzi
wa Utawala na Rasilimaliwatu Wizarani, Idara za Serikali
zinazojitegemea, Taasisi za Umma na Makatibu Tawala Wasaidizi Sehemu ya
Utawala na Rasilimaliwatu katika Sekretariati za Mikoa na Mameneja
Rasilimaliwatu katika Wakala la Serikali wakimsikiliza mgeni rasmi
Balozi Ombeni Sefue (haypo pichani) wakati wa ufunguzi wa mkutano huo
katika ukumbi wa St. Gasper mjini Dodoma leo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...