KLABU
ya mchezo wa Pool ya Blue Leaf Mkoani Lindi imemefanikiwa kutwaa
Ubingwa wa fainali za mashindano ya mchezo huo yajulikanayo kama “Safari
National Pool Competition 2014” uliomalizikamwishoni mwa wiki Mkoani
humo na kuzawadiwa pesa taslimu Shilingi 800,000/= pamoja na tiketi ya
kuwakilisha Mkoa wa Lindi kwenye fainali za zinazotarajiwa kufanyika
Mkoani Kilimanjaro.
Nafasi
ya pili ilichukuliwa na Bwalo la Polisi Pool Klabu na kuzawadiwa fedha
taslimu Shilingi 400,000/= na nafasi ya tatu ni Fisi Pool Klabu ambao
walijinyakulia fedha taslimu Shilingi 250,000/=
Upande
wa mchezaji mmoja mmoja wanaumeHassan Salum alifanikiwa kutwaa ubingwa
wa mkoa na kuzawadiwa fedha taslimu Shilingi 400,000/= na nafasi ya pili
ilichukuliwa na Pius Abubakari ambaye alizawadiwa Shilingi 250,000/=
Mchezaji
mmoja mmoja Wanawake, Mwajuma Othman alifanikiwa kutwaa ubingwa huo na
kuzawadiwa fedha taslimu Shilingi300,000/= pamoja na kuwakilisha mkoa
katika fainali za kitaifa upande wa wanawake.Nafasi ya pili ilichukuliwa
na Mariam Hassan ambaye alizawadiwa fedha taslimu Shilingi 200,000/=.
Fainali
za kitaifa za 2014 za “Safari National Pool Competion” zinatarajiwa
kufanyika Moshi Mkoani Kilimanjaro kwa kushilikisha Mikoa 17 ambayo ni
Tabora,Shinyanga,DodomaMbeya,Iringa,Morogoro,Mwanza,Kagera,
Manyara,Arusha,Tanga,Pwani,Ilala,Lindi,Temeke,Kinondoni na wenyeji wa mashindano kwa mwaka huu mkoa wa Kilimanjaro.
Manyara,Arusha,Tanga,Pwani,Ilala,Lindi,Temeke,Kinondoni na wenyeji wa mashindano kwa mwaka huu mkoa wa Kilimanjaro.
Bingwa
wa mchezo wa Pool Afrika upande wa mcvhezaji mmoja mmoja
Wanaume(Singles), Patrick Nyangusi (kushoto) na Salum Ally wakishindana
kucheza(Lag) wakati wa fainali za mchezo huo upande wa mchezaji mmoja
mmoja wanaume uliochezwa katika klabu ya Jambo Lee Kawe jijini Dara es
Salam mwishoni mwa wiki.Partick Nyangusi alishinda mchezo huo.
Mchezaji
wa Klabu Pool ya Jaba, Kinondoni Dar es Salaam, Mayaula Muhagama
akicheza wakati wa fainali zamchezo huo za mashindano yajulikanayo kama
‘Safari National Pool Competition 2014” ngazi ya Mkoa,yaliyofanyika
katika Klabu ya Jambo Lee Kawe Dar es Salaam.Kulia ni Mwamuzi wa mchezo
huo, Peter Majani.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...