WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo Dk. Fenella Mukangara keshokutwa anatarajiwa kuzindua Siku ya Msanii Tanzania katika sherehe zitakazofanyika katika hoteli ya Sea Cliff Dar es Salaam. Akizungumza jana mjini Dar es Salaam, Ofisa Habari wa Mradi wa Siku ya Msanii Tanzania, Petter Mwendapole, alisema Dk. Mukangara amepewa jukumu hilo kutokana wizara yake kuhusika moja kwa moja sanaa. “Waziri amekubali jukumu la kuwa mgeni rasmi kwa sababu wizara yake ndio mama wa wasanii, na anaelewa matatizo ya wasanii na amekubali kuwa kulibeba jukumu hilo na atakuwepo na timu nzima ya wizara,” alisema. Mkurugenzi wa Masoko wa Basata wa Vivian Shaluwa alisema siku ya Msanii ilibuniwa mwaka 2004 lakini Tanzania iliamua kuichukua na kuianzisha mwaka 2008 lakini baada ya mchakato wa muda mrefu, kampuni ya Haak Neel imepewa jukumu la kusimamia kazi hiyo. 
“Siku ya Msanii itahusisha sanaa mbalimbali kuanzia urembo, muziki wa dansi, uchoraji, unenguaji, lakini pia siku ya Msanii ambayo tamati yake itakuwa Oktoba 25 itakuwa na tuzo za aina mbalimbali kutambua mchango wao,” alisema. 
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Haak Neel Production, Godfrey Katula alisema kampuni yake imejiandaa vyema kusimamia shughuli hiyo na kuwataka wadau mbalimbali kuhakikisha wanatumia vyema siku ya Msanii katika kutambulisha kazi. 
“Haak Neel imejipanga kushirikiana na wasanii katika kutambua siku yao, tumeona kuna siku ya wanawake duniani, kuna Mei Mosi, kwa ajili ya wafanyakazi, kuna siku ya ukimwi kwa hiyo hii ni heshima kwa wasanii kutambuliwa kwa siku yao.” 
Mbali na viongozi wa BASATA, Kamati ya Siku ya Msanii inahusisha wasanii kutoka sekta mbalimbali za sanaa ambao ni pamoja na Philemon Mwasanga, Asia Idarous, Kimera Billa, Abdul Salvador, Adrian Nyangamale, Sulemani Ling’ate.
 Mkurugenzi wa Masoko wa BASATA, Vivian Shalua akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari.  Ofisa Habari wa Msanii Day, Peter Mwendapole waliokaa wa kwanza kulia akizungumza  na waandishi wa habari juu ya siku hiyo.
Mkurugenzi wa Masoko wa Baraza la Sanaa Tanzania ( Basata ),Vivian Shalua akiongea na waandishi wa habari juu ya siku ya Msanii Tanzania. Kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Haak Neel Production Godfrey Katula akifuatiwa na Ofisa habari wa Msanii Day, Peter Mwendapole na Ofisa Masoko wa Msanii Day Catherine Metili (kulia) na wajumbe wengine.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...