Mfuko
wa Fursa Sawa kwa Wote (EOTF) utaendesha mafunzo ya siku tatu -Jumatatu
23 -Jumatano 25 Juni 2014, katika ukumbi wa Mabati Jeshi la Kujenga
Taifa Mgulani, Temeke, jijini Dar es salaam.
Lengo
la mafunzo haya kwa mwaka huu ni kuwaelimisha na kuwawezesha wanawake
wajasiliamali jinsi ya kupata mitaji, masoko na kufanya biashara
endelevu.
Mada
kuu zitahusu: Uwekezaji na Ukuazaji mtaji, Mtaji sio Lazima Uwe Fedha;
Utunzaji wa Kumbukumbu za Biashara yako, Kuwaunganisha Wazalishaji na
Masoko; Mnyororo wa Bidhaa; Mbinu za kushiriki Maonyesho ya Biashara,
Usindikaji na Mazao, Usajili na Matumizi ya “Bar Code” na
Elimu na uhamasishajiwa wa maradhi sugu na hatari kwa wanawake
yanayorudisha Maendeleo yao – Saratani ya Matiti na Shingo ya Kizazi,
Fistula, UKIMWI, Dengue/Malaria na Homa ya Ini.
Watoa
Mada ni pamoja na Wajasiriamali maarufu - IPP, Soko la Hisa la
Dar-es-salaam- DSE, Wakufunzi kutoka TRA, TanTrade Chuo Kikuu cha
Dar-es-salaam, Madaktari Kutoka CCBRT, Ocean Road, Ilala na Temeke .
Wanawake
wote mnakaribishwa kuhudhuria Mafunzo haya yenye lengo la kuwakomboa
kiuchumi, Kiafya na kuwakutanisha kubadilishana ujuzi, Uzoefu na
biashara.
Hakuna malipo kwa kushiriki.
KARIBUNI
Mkurugenzi Mtendaji,
Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote (EOTF).
0715 263284
DAR ES SALAAM
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...