Tunapenda kutoa taarifa kwamba ile timu tishio upande wa veterans hapa nchini yaani Golden bush veterans ambao ndio mabingwa wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yaani Bara na visiwani watakuwa Makamboko siku ya tarehe 22 June 2014 kwa mualiko wa Makambako Veterans wakishirikiana na Serengeti Breweries.
Mwaliko huu umetokana na historia ndefu ya timu yetu ambayo imejijengea heshima ya kuwa na ushirikiano wa karibu na timu nyingi za veterans wakiwemo Makambako Veterans ambao ndio watakuwa wenyeji wetu siku ya tarehe 22. Aidha tunapenda kutumia nafasi hii kama sehemu mojawapo ya kutengeneza urafiki wa karibu Zaidi na timu za nyanda za juu kusini.
Maandalizi yamekamilika kwa asimia 95 ambapo mkuu wetu wa msafara bwana Waziri Mahadhi Mandieta akishirikiana na mwenyekiti wa kamati ya ufundi bwana Yahaya Issa wanakamilisha baadhi ya mambo madogo madogo tayari kwa safari ya kuelekea mkoani Njombe.
Kesho tutakuwa na mechi ya kirafika na Wizara ya afya ikiwa na sehemu mahususi kabisa ya kupasha misuli kabla ya kuanza safari ndefu kabisa ya kuelekea Makambako. Karibuni sana, game ya kesho itapigwa katika uwanja wa Kinesi ali maarufu kama St James’ park kuanzia saa saa mbili kamili asubuhi.
Asanteni sana kwa kunisikiliza.
Onesmo Waziri “Man of the match” “Ticotico” “player Maker” Msemaji wa timu na Mchezaji Mwandamizi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...