Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bw. John
Haule akipanda mti katika kuashiria kuadhimisha Siku ya Mazingira
Duniani katika eneo la Kituo wa Mikutano cha Kimataifa cha Julius
Nyerere (JNICC) kilichopo jijini Dar es Salaam. Siku hiyo iliadhimishwa
duniani kote tarehe 05 Juni, 2014.
|
Afisa
Mambo ya Nje, Bi. Naomi Zegezege akipanda mti kwa niaba ya Wafanyakazi
wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa katika kuadhimisha
Siku ya Mazingira Duniani.
|
Bw.
John Haule akiongozana na Mkurugenzi wa Kituo cha Mikutano cha
Kimataifa cha Julius Nyerere Bw. Deus Kulwa (kulia) baada ya kupanda
miti katika kuadhimisha siku ya mazingira duniani. Kushoto ni Bi Naomi
Zegezege, Afisa Mambo ya Nje
|
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bw. John
Haule akizungumza na Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje pamoja na
Wafanyakazi wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere
(hawapo pichani) wakati wa maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani.
|
Baadhi Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wakimsikiliza Katibu Mkuu (hayupo pichani)
|
Katibu Mkuu, Bw. John Haule na Mkurugenzi wa JNICC, Bw. Kulwa katika picha ya pamoja.
|
Katibu
Mkuu akiwa katika picha ya pamoja na Watumishi wa Wizara ya Mambo ya
Nje na Ushirikiano wa Kimataifa baada ya Wizara kuadhimisha Siku ya
Mazingira Duniani kwa kupanda miti.
|
Bw. John Haule akizungumza na waandishi wa habari
Picha na Habari na Reginald Philip
Wizara ya Mambo ya Nje yaadhimisha Siku ya Mazingira Duniani
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bw. John
Haule, amewataka wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Kimataifa na watanzania wote kwa ujumla kutumia nishati endelevu badala
ya kuni na mkaa, kuunga mkono juhudi za serikali za kunusuru mazingira.
Akiongea
katika maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani yaliyoandaliwa na
wizara kwenye ukumbi wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo, Bw.
Haule alisema hatua nyingine za kutunza mazingira ni kupanda miti;
kutolima kwenye miteremko ya milima; kupunguza matumizi makubwa ya
mbolea na kuachana na matumizi ya mifuko ya plastiki isiyiteketezeka kwa
urahisi.
Wawekezaji katika viwanda watumie teknolojia ya kisasa isiyoongeza gesi joto, alishauri.
Katika maadhimisho hayo chini ya kauli mbiu isemayo “Sayari ya dunia ni kisiwa chetu wote kwa hivyo tuunganishe nguvu zetu kulinda kisiwa hiki,” Bw.
Haule alipanda mti kuanzisha mpango wa wizara wa kupanda miti kutunza
mazingira. Miti saba ilipandwa nje ya ukumbi wa Julius Nyerere leo kwa
kuanzia.
Maadhimisho hayo pia yalishirikisha wafanyakazi wa AICC na ukumbi wa Julius Nyerere.
|
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...