Jamhuri ya Guinea ya Ikweta ni nchi iliyopo magharibi Afrika ya Kati. Ni nchi mojawapo ndogo kwa bara la Afrika.Imepakana na Kamerun upande wa kaskazini, Gabon kusini na mashariki, na Guba la Guinea magharibi, ambapo kisiwa cha São Tomé na PrÃncipe chapatikana kusini-magharibi mwa Guinea ya ikweta.
Ilikuwa koloni ya Uhispania ambapo iliitwa Guinea ya Uhispania, na eneo zake ambazo zajulikana (kwa bara kama RÃo Muni) za husu eneo kadhaa visiwa, na pia kisiwa kama Bioko ambapo mji mkuu humo, Malabo (ambayo iliitwa, Santa Isabela).
Jina la nchi hii latokana na kuwa ya kwamba imo karibu na Ikweta na pia karibu na Guba la Guinea.
Ni nchi pekee Afrika ambapo lugha ya Kihispania ndio lugha rasmi na ya Taifa, hasa ukiacha maeneo ya Hispania iliozungukwa na bara, Ceuta na Melilla na nchi-Isiotambuliwa-kimataifa Jamhuri ya Sahara ya Kidemokrasia ya Kiarabu.
Malabo ni mji mkuu wa Guinea ya Ikweta mwenye wakazi takriban 90,000 - 100,000. Iko mwambaoni wa Atlantiki kwenye pwani la kaskazini ya kisiwa cha Bioko (zamani: Fernando Po).
Mji ulianzishwa kwa jina la Port Clarence kuanzia 1827 na Waingereza waliokuwa wamekodi kisiwa cha Fernado Po kutoka kwa Hispania. Uingereza ulitumia kisiwa kama kituo cha jeshi la uanamaji lilizozunguka Atlantiki kwa shabaha ya kukomesha biashara ya watumwa.
Waingereza walipeleka hapa watumwa waliopatikana kwenye meli za bishara ya watumwa.
Mwaka 1843 Waingereza walihamisha kituo chao ch kijeshi kwenda Sierre Leone na sehemu ya watumwa wa zamani waliopewa uhuru wao walibaki wengine wakafuatana na Waingereza kwenda Sierra Leone.Wahispania walirudi polepole wakabadilisha jina la mji kuwa Santa Isabel.
Tangu uhuru wa Guinea ya Ikweta mwaka 1968 Santa Isabel ikawa mji mkuu. Wakati wa utawala wa rais Francisco MacÃas Nguemajina lilibadilishwa kuwa Malabo.
Malabo ni kitovu cha kiuchumi cha nchi. Mazao ya kakao, kahawa na ubao yanapelekwa hapa kwa meli na kuuzwa nje.Na mji huo umeendelea kushamiri kutokana na bisahara ya gesi na mafuta yanayopatikana kwa wingi nchini humo, katika himaya yake ya bahari ya Atlantiki.
![]() |
Ni ajabu lakini ni kweli kwamba mji wa Malabo ambao ni kisiwa uko mbali kabisa na nchi yake ya Guinea ya Ikweta ama Equatorial Guinea kama ramani inavyoonesha |
Kutokana na utajiri wa gesi na mafuta jiji la Malabo linamandhari hii kila mahali. Hali ya hewa hapa ni kama Zanzibar, ila kuna mvua za mara kwa mara na radi mtindo mmoja. Cheki huko juu kulivyonuna...
Miundo mbinu yake si mchezo
Pia ni wapenzi wa utamaduni
Ankal alikuwa huko hivi majuzi. Hapa ni nje ya Ukumbi wa Mikutano wa kimataifa wa Sipopo. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA
Shukrani sana bwana michuzi kwa taswira hizo.Kwa maoni yangu kama walivyo fanya wao hata sisi tunaweza isipokuwa kuna hitaji kujitambua kwanza kwa kufanya mageuzi ktk sheria zinazo simamamia natural resources zetu ili ziweze kuwanufaisha watanzania wote.makosa tuliyoyafanya huko nyuma ya kushindwa kusimamia mapato ya migodi yetu yasirudiwe katika Gasi asilia.
ReplyDeletePolepole na kwa kudra za Mwenyezi Mungu basi nasi tutafika hapo walipo wenzetu..ni hatari lakini ni salama. .bongo itafika tuu..uzuri sisi bongo tumeanza kujipanga sehemu zote na hivyo tukisimama ni moja kwa moja kama mtoto wa twiga..hatuli nyasi bali matawi. ..juju kwa juu kaka..
ReplyDeleteMdau wa kwanza na wa pili mna mawazo mazuri lakini ili bongo tufike huko tunahitaji kujitambua kifikra kwanza. Miji hii hii tuliyo nayo ingeweza kuwa na madhari kama hizo lakini kwa vile hatujitambui, tumeshindwa kuifanya hivyo. Hata kama tutarudisha pesa zote za gesi na madini hapa nyumbani kama watu hawatakuwa na hulka ya kupenda vitu vizuri, kutunza mazingira kamwe hatutafiko huko waliko wenzetu.
ReplyDeleteHahaha safi sana
ReplyDeleteAnkal naona wapenda sana vakesheni. Mimi pia napenda kusafiri lakini sina mbavu.Basi nauliza kama unahitaji pota wakukubebea mizigo kwenye safari zako.
ReplyDeleteSisi miji yetu hasa mikoani tunahitaji kujifunza kutokana na taswira hizi tunapopanga kuendeleza miji yetu. Ni pazuri Malabo.
ReplyDeleteBongo tunazubaa kupanga miji mpaka wananchi wanaenda kujenga kiholela kwa sababu ya kuongezeka kwa idadi ya watu halafu ndiyo tunarudi kupanga kwanza kwa njia ya kuwabomolea ili kuwe na mpango na barabara. Kwanini miji haipangwi ikiashiria ukuaji wa idadi ya watu..
ReplyDeletekwani viongozi wetu wakitembelea hizo nchi za wenzetu hawaoni haya maendeleo na kujisikia aibu.
ReplyDeleteAnka umetoka chicha ! si mchezo
ReplyDeletewadau FFU
Aisee nikuzuri sanaa. Panapendeza na panavutia sana.
ReplyDeletewatanzania na viongozi wao wanasubir gesi,eti ndio wataendelea.Madini yameisha,mashimo yamebaki ni mmefika wapi?
ReplyDeletekila kukicha viongozi ni misemina na mikutano ambayo haina tija.Angalia michuzi kila leo,serikali inatumia hela nyingi sana kwenye mikutano,semina na magari.
Tanzania inahitaji kiongozi ambaye atakuwa na fikra tofauti,ila kwa mwendo huu hata huko simpopo hatutawafikia.
Something is very wrong with us indeed.
Nimekaa Malabo na Bata, hizo Ghorofa hapo ni ukiwa unatoka airport kuelekea mjini zimejengwa kwa amri ya Rais kuwa watu wasione umaskini ulio nyuma ya hizo nyumba.
ReplyDeleteMaji ni tatizo na umeme ni wa mgao, wananchi wa EG wanaishi kimaskini sana, nyinyi mlioenda kwa siku tatu kamwe hamtaweza kuona hali halisi ya maisha.
Tanzania is much better kwa ujumla.