Na Sultani Kipingo
Kamati ya
maandalizi ya Kombe la Dunia 2014 ilikuwa na nyota watano wa zamani wa Brazil
(pichani wakiwa na maafisa wa chama cha soka cha Brazil) waliowahi kuwika
katika michuano hiyo tokea mwaka 1958 ilipofanyika nchini Sweden. Kamati hiyo,
iliyoundwa January 2013 inaundwa na wachezaji wakongwe kina kutoka kushoto juu:
Amarildo Tavares da
Silva (wa tatu toka kulia) , José Roberto Gama de Oliveira
(Bebeto), Carlos Alberto
Torres, Marta Vieira da
Silva, Ronaldo Luis
Nazario de Lima (wa pili kulia) na Mário Jorge Lobo Zagallo (kushoto).
Watano kati ya
wanakamati hao ambao wamepewa Ubalozi wa FIFA waliwahi kuchezea Brazil wakati
nchi hiyo ilipofanikiwa kunyakuwa kombe hilo la dunia. Nao ni Mário Zagallo (mwaka 1958 nchini Sweden), Amarildo (waka 1962 nchini Chile), Carlos Alberto (mwaka 1970 nchini
Mexico), Bebeto (waka 1994 nchini
Marekani), na Ronaldo (mwaka 2002 nchini Korea ya
kusini na Japan).
Balozi mwingine ni
mwanamama Marta Vieira da
Silva ambaye ni mshindi mara 5 wa tuzo ya Mchezaji Bora wa FIFA kwa
wanawake katika miaka ya 2006, 2007,
2008, 2009 and 2010.
Ronaldo alisema
baada ya kuteuliwa: “Ni muhimu tukawa makini maana mbele yetu tuna kazi ya
kuangalia maendeleo ya ujenzi wa viwanja, kuchagua mahali ambapo timu ya Taifa
itapiga kambi na viwanja mahususi vya mazoezi, na pia kufikia maamuzi muhimu ya
kihistoria kama vile kuzindua kauli mbiu ya michuano na Mwanasesera wa Kombe la
Dunia la FIFA.”
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...