"Brazuca" si kitu kingine bali ni jina la mpira unaotumika katika
michuano ya Kombe la Dunia inayoendelea chini Brazil hivi sasa.
Neno hilo lina
maana mbili. Ya kwanza ni neno la nchi hiyo kwa wa-Brazil wanaoishi nje ya nchi
– yaani Diaspora. Maana ingine, neno hilo lina maana ya kujivunia, kuufurahia na kutambia u-Brazil kwa watu wa nchi hiyo, ama
kitu ama jambo lolote la kusisimua linalohusiana na nchi hiyo.
Baadhi
ya mipira ya Kombe la Dunia imekuwa maarufu kuliko mingine, huku wachezaji wakiilalamikia
kwa kile wanachosema mipira hiyo husafiri kwa kasi zaidi hewani, kiasi hata
kusumbua walinda milango
Adidas, watengenezaji maalumu wa mipira kwa ajili ya Kombe la
Dunia tokea mwaka 1970, waliuita “Jabulani” mpira uliotumika katika fainali
hizo mwaka 2010 huko Afrika Kusini, na kulakiwa na kila aina ya makelele kuwa
mwendo wake hautabiriki.
Huu wa sasa
jina lake rasmi ni "Adidas Brazuca" na umetengenezwa na kampuni ya Forward Sports
ya
Sialkot nchini Pakistan. Jina “Brazuca” la mpira huo lilizinduliwa September 2,
2012 jijini Rio de Janeiro, kupitia kura ya maoni iliyoendeshwa na Fifa na
Adidas, ambapo wapiga kura zaidi ya milioni moja wa Brazil walilichagua kwa
kura 77.8% dhidi ya majina mengine mawili yaliyopendelkezwa – “Bossa Nova
(14.6%) na Carnavelesca (7.6%)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...