Napenda kuwajulisha marafiki zangu wote kwamba akaunti yangu ya facebook ime-hackiwa na kuanza kutuma ujumbe kwa marafiki zangu kuwataka waingie kwenye link kwani nina maongezi ya siri.

Tafadhali puuzia ujumbe huo kwani utasababisha akaunti yako nayo ku-hackiwa.
Tafadhali sambaza ujumbe huu, wakati tunaendelea kujaribu kuiokoa. Nawaomba radhi wote walopatwa na usumbufu huu.
Asanteni sana
- Jerry Silaa

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Pole sana ndg yangu!Post ya mwisho niliyoona toka kwako ni ya Web ya VICOBA.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 16, 2014

    Welcome fast in Tanzania Cyber Crime Laws!!!

    Tutokoma maana tupo uchi mbele za wapenda kujua vya watu kama hackers.

    Zaidi ya kilio cha Mstahiki Meya Silaa idadi kubwa ya watu Taarifa zao za siri kama Mawasiliano ya Simu na Akaunti za Benki zipo mashakani huku Wahalifu wakitumia upungufu wa kutokuwepo Sheria za Makosa ya Kimtandao nchini.

    Jamaa mmoja anasikitishwa kuona taarifa zake za kibenki zinafahamika na watu bila ridha yake.

    Mfano Wahalifu na waingiliaji hawa wana panga na Makarani wa Benki wasio waaminifu na kutoa taarifa zake kwao, jamaa hadi hata siku akiweka fedha ktk Akaunti zakem wanajua !

    Hadi idadi kamili ya fedha zake Benki wanajua !

    Hii ni hatari sana watu kuweza kuingilia Privacy za watu kirahisi!!!

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 17, 2014

    Mdau wa Pili:

    Hizi Sheria ni muhimu ziletwe haraka, unapoona mtu anafuatiliwa kwa taarifa za Kifedha na Mawasiliano kama hizo za Benki na Mitandao ujue hapo pana moja kati ya mabalaa haya hapa chini:

    1.Wahalifu na maadui zako wanataka kukuchafua ktk jamii,

    2.Wahalifu na maadui zako wanataka kukukopa au kukuhujumu,

    3.Wahalifu na maadui hao hawana nia njema kabisa , kwa kuwa ya nini ujue undani wa mtu kiasi hicho?

    Hili la usiri wa taarifa za watu ama kweli ni balaa la aina yake kumuingilia mtu Muheshimiwa Kiongozi anaye heshimika kwenye jamii kama Meya huyo mtu au watu wanatafuta nini jamani?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...