Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mafuta na Gesi ya Swala (Tanzania) PLC, David Mestres Ridge
(kulia), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, kuhusu ufunguzi wa
ofa ya awali kwa umma ijulikanayo kwa kifupi (IPO) ambayo itakuwa na hisa za kawaida,9,600,000.
Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa ARCH Financial $ Investment Adivisory Limited,Iyen Nsemwa.

Mkurugenzi wa Kampuni ya Mafuta na Gesi ya Swala (Tanzania) PLC, Abdullah Mwinyi (katikati), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, kuhusu ufunguzi wa ofa ya awali kwa umma ijulikanayo kwa kifupi (IPO) ambayo itakuwa na hisa za kawaida,9,600,000. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Swala, David Mestres Ridge na Mkurugenzi Mkuu wa ARCH Financial $ Investment Adivisory Limited,Iyen Nsemwa. (Na
Mpiga picha Wetu)
Kampuni ya Mafuta na Gesi ya Swala
(Tanzania) Plc leo imetangaza ufunguzi wa ofa yake ya awali kwa umma ijulikanavyo kwa
kifupi kama ("IPO") yenye hisa za kawaida 9,600,000. Kampuni itakuwa ikiuza kila hisa
kwa bei ya shilingi za Kitanzania 500 kuanzia tarehe 9 juni 2014 mpaka tarehe 4 Julai 2014.
Tangazo hili limekuja wiki moja baada ya kampuni kupokea idhini yake rasmi kutoka Mamlaka
ya masoko ya Mitaji na Dhamana Tanzania ("CMSA"), na kuifanya kuwa ni ofa ya kwanza
kufanyika kwenye sekta ya mafuta na gesi katika ukanda wa Afrika Mashariki.
Mkurugenzi Mtendaji wa Swala Bwana David Mestres Ridge alisema, "Tunafuraha
kuwa, leo Kampuni ya mafuta na gesi ya Swala (Tanzania) Plc imezindua rasmi mpango wake
wa ofa ya awali kwa umma ijulikanayo kama IPO. Hii ni hatua kubwa si tu kwa ajili ya Swala
lakini pia kwa Tanzania na watu wake kwa ujumla. . Kuwekeza hisa katika mafuta na gesi ni
moja ya njia za kupanua wigo wa kiuchumi kwa mtu yeyote na inaruhusu mtu yeyote kumiliki
hisa katika biashara hii inayokua kwa kasi ".
Bwana Ridge alizidi kusema, "Tunaishukuru sana Serikali ya Tanzania, Shirika la mafuta
na gesi Tanzania (TPDC), Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA) kwa kuturuhusu
kuwa kampuni ya kwanza ya Mafuta na gesi katika Afrika Mashariki inayomilikiwa na umma.
Kwa niaba ya wakurugenzi wote wa Swala napenda kuukaribisha rasmi umma kuwekeza katika
Kampuni ya mafuta na gesi ya Swala (Tanzania) Plc ".
Mhe. Abdullah Mwinyi, ambaye ni Mkurugenzi wa Swala Tanzania Plc
aliongeza, "Kumekuwa na mjadala mkubwa kwa wazawa katika sekta hii ya uchimbaji wa
mafuta na gesi; Tumefurahia kwamba leo kampuni ya mafuta na gesi ya Swala imekuwa ya
kwanza kuanza utekelezaji wa haja za wazawa katika sekta hii ya mafuta na gesi. Tunaamini
kwa dhati kabisa kwamba Watanzania wapewe nafasi ya kushiriki katika biashara ya mafuta na
gesi; ufunguzi huu wa IPO unaruhusu wao kufanya hivyo."
Fomu za maombi na nakala ya Waraka wa matarajio zitakuwa zinapatikana katika ofisi
zote za Mawakala wenye leseni kutoka soko la hisa la Dar Es Salaam (DSE) walioko karibu
yako, matawi ya Benki ya CRDB Plc na ofisi za Arch Financial & Investment Advisory Ltd.
Ofa
iko wazi kuanzia tarehe 9 Juni 2014 mpaka 4 Julai 2014. Kwa sasa hakuna ukomo wa kiwango
cha juu cha hisa, lakini kiwango cha chini cha kununua ni hisa 100 kwa mtu. Waraka wa
Matarajio wa kielektronikia unapatikana kwenye tovuti ya kampuni www.swala-energy.co.tz au
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...